Na Is-haka Omar, Zanzibar.
WAZIRI Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Mh. Kassim Majaliwa kesho Novemba 25, mwaka huu anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi katika mashindano ya fainali ya ligi za Majimbo ya Mkoa wa Mjini
Zanzibar.
Mchezo
huo utakaotimua vumbi katika Kiwanja cha Amaan Stadium Unguja, ambapo
utazikutanisha timu mbili zilizofanikiwa kufika finali ambazo ni Timu ya Afisi
Kuu CCM Zanzibar na Timu ya Jimbo la Kwahani.
Kabla
ya mtanange huo mkali kutatanguliwa na mechi ya kumsaka mshindi wa tatu ambayo
itachezwa na timu za jimbo la Kikwajuni na jimbo la Malindi kwa ajili ya
kutafuta mshindi wa tatu.
Michezo
hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkali kutokana na uwezo wa kila timu
katika masuala ya Soka.
Akizungumza
na mwandishi wa Habari hizi Katibu wa Kamati ya mashindano hayo, Suzan Kunambi
amesema maandalizi ya fainali hiyo tayari yamekamilika kwa upande wa Kamati
yake na kwa timu zinazotarajiwa kushiriki zote zimedhibitisha ushiriki wao.
Ameeleza
kwamba mashindano hayo yaliyoanza mwezi Machi 24 mwaka huu kwa kuzishirikisha
timu 18 za majimbo pamoja na vikundi vya uhamasishaji vya CCM kutoka Mkoa wa
Mjini pamoja na majimbo jirani yaliyoalikwa kutoka Mikoa yote ya Unguja.
Katibu
huyo amefafanua kuwa mashindano hayo yalizinduliwa na Makamo Mwenyekiti
wa CCM Zanzibar ambaye pia ni Rais wa Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein na
yanatarajiwa kufungwa na Waziri Mkuu wa Serikali ya Jamhuri ya muungano wa
Tanzania Mh. Kassim Majaaliwa.
Suzan
ameyataja malengo ya mashindano hayo kuwa ni kujenga umoja na mshikamano kwa
vijana mbali mbali waliopo majimboni ili wajikwamue katika changamoto za
ukosefu wa ajira na makundi maovu kwa kujiajiri wenyewe kupitia vipaji vyao vya
soka.
Amesema mashindano hayo yamekuwa ni chachu ya kuibua vipaji vya soka ambapo
wacheza mbali mbali wamepata fursa za kujiunga na timu kubwa zilizopo katika
mashindano ya ligi za madaraja mbali mbali ya soka nchini.
“
Tunamshukru Makamo Mwenyekiti wetu Dk. Shein kwa mchango wake mkubwa wa
kuthamini soka la vijana na kuimarisha sekta ya michezo nchini”, alitoa pongezi
hizo Katibu huyo na kuongeza kuwa Kamati hiyo imejipanga kushirikisha timu
nyingi zaidi ili mashindano yaendelee kuwa bora na kuwanufaisha vijana.
Akizungumzia
zawadi zitakazotolewa kwa mshindi wa mwanzo hadi wa tatu amefafanua kuwa mshindi wa
kwanza atapata Gari moja, Kikombe na medali ambapo mshindi wa Pili atapata
fedha taslim shilingi milioni tatu na medali pamoja na mshindi wa tatu atapata
shilingi milioni mbili na medali.
Sambamba
na hayo aliwaomba wapenzi wa Soka wa ndani na nje ya Zanzibar kujitokeza kwa
wingi katika uwanja wa Amaan kushangilia timu zao kwani kiingilio ni bure.
Mechi
ya mwanzo itachezwa majira ya saa 8:00 mchana na ya pili ambayo ni fainali
itachezwa kuanzia majira ya saa 10:00 jioni.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni