Na Is-haka Omar, Zanzibar.
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa
ameeleza kuwa mchezo wa soka ni miongoni mwa masoko huria linatoa nafasi kwa
vijana nchini kujiajiri wenyewe.
Akihutubia mamia ya wapenzi wa soka katika
fainali za mashindano ya majimbo ya Unguja kwa mchezo huo iliyofanyika katijka uwanja
wa michezo wa Amaan Zanzibar.
Amesema mchezo huo umekuwa maarufu ulimwenguni
na unatoa fursa mbali mbali kwa vijana ambao wana vipaji vya mchezo huo.
Aidha Mhe. Majaliwa amepongeza
waandaaji wa mashindano hayo kwa kubuni mashindano la kuwakutanisha vijana
katika jukwaa moja kupitia sekta ya michezo bila kujali tofauti zao kisiasa
kiuchumi na kijamii.
Waziri Mkuu Majaliwa ambae pia ni
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa, amesema CCM imekuwa ni mlezi bora wa kulea
makundi mbali mbali ya kijamii hususani vijana ambao kitakwimu ni wengi kuliko makundi
mengine na kuwataka wawe na maadili mema yatakayosaidia kukuza sekta za
utamaduni na uchumi.
Ametoa wito kwa majimbo mbali mbali
ya CCM kwa upande wa Tanzania bara kuiga
mfano wa majimbo ya Zanzibar kwa kuandaa
mashindano ya michezo mbali mbali kwa vijana ili kuibua vipaji vitakavyoendelea
kuijenga heshima ya nchi kimichezo
katika anga za kimataifa.
“Kupitia mchezo huu nimeona vijana wengi
wenye vipaji wanaoweza kucheza katika timu kubwa zilizopo nchini, hivyo
endeleeni kujitokeza na kushikamana na michezo ili kujiepusha na vikundi viovu
kwani mtapoteza muelekeo wa maisha yenu’’, alisema Waziri Mkuu Mhe. Kassim
Majaliwa.
Mapema Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk.
Abdulla Juma Mabodi alisema mchezo huo
umeongeza mahusiano mema kwa majimbo
yote yaliyoshiriki katika mashindano
hayo.
Dk. Mabodi alisema CCM kitaendele
kuwa karibu na waandaji wa mashindano hayo
katika ligi zijazo kwa lengo la kudumisha amani, utulivu na mahusiano
mazuri kwa vijana nchini.
Mashindano hayo yalianza kutimua
vumbi toka mwezi Mach 24 mwaka huu yalizinduliwa na Makamo Mwenyekiti wa CCM
Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein yakiwa na timu 18 za Majimbo ya Unguja.
Katika fainali hiyo timu ya Afisi Kuu
CCM Zanzibar imefanikiwa kutwaa ubingwa wa mashindano hayo baada ya kuifunga
timu ya Jimbo la Kwahani magoli 3 – 1 yaliyofungwa na Kheir Makame mnamo dakika
za 25, 32 na Haidham Khamis ksatika dakika ya 65 wakati goli la Kwahani
lilifngwa na Yusuf Juma katika dakika ya
15.
Kufuatia ushindi wa timu ya Afisi Kuu CCM
Zanzibar, Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Mabodi amewapongeza wachezaji
wa timu ya Afisi Kuu kwa kutwaa ubingwa huo na kuipa zawadi ya shilingi Milioni
tano.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa (kushoto) akikabidhi Gari ndogo aina ya Carry kwa nahodha wa timu ya Afisi Kuu CCM Zanzibar, Vuai Makame Jecha. |
Spika wa Baraza la Wawakilishi
Zanzibar Mhe. Zubeir Ali Maulid akikabidhi zawadi ya mchezaji bora wa
mashindano ya majimbo nahodha wa timu ya Afisi Kuu CCM Zanzibar Vuai Makame
Jecha. |
Viongozi mbali mbali wa Serikali na CCM wakiwa jukwaa kuu la Uwanja wa Amaan Stadium wakifuatilia mchezo huo. |
Baadhi ya wananchi waliojitokeza katika uwanja wa Amaan kuangalia mechi hiyo wakifuatilia kwa makini timu zao. |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni