Alhamisi, 18 Oktoba 2018

MATUKIO KATIKA PICHA MKUTANO WA KAMPENI ZA CCM JANG'OMBE UWANJA WA KWAALINATU-18/10/2018.


 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar  Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' akimnadi Mgombea wa CCM nafasi ya Uwakilishi Jang'ombe  Ndugu Hamza Ramadhan Chande kupitia Mkutano wa Kampeni uliofanyika Uwanja wa Kwaalinatu Zanzibar.

 MGOMBE wa Uwakilishi kwa Tiketi ya CCM katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Jang'ombe Ndugu Ramadhan Hamza Chande akiomba kura za ndio kwa Wana-CCM wa maeneo ya Kwaalinatu na Jang'ombe kwa ujumla.

 MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa Mjini Ndugu Talib Ali Talib akizungumza na kuomuombea kura Mgombea wa CCM wa Nafasi ya Uwakilishi Ndugu Ramadhan Hamza Chande.

 MBENGE wa Jimbo la Kikwajuni Mhe. Hamad Yussuf Masauni akimuombea kura Mgombea Uwakilishi wa Tiketi ya CCM kupitia Mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Kwaalinatu.

 MBUNGE wa Jimbo la Kiembe samaki  Unguja Mhe. Ibrahim Raza akimuombea kura Mgombea Uwakilishi wa tiketi ya CCM Ngdugu Ramadhan Hamza Chande kupitia Mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Kwaalinatu.

 MBUNGE wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Abdullah Hasnuu Makame akizungumza katika Mkutano huo wa kampeni na kumuombea kura Mgombea Uwakilishi wa Tiketi ya CCM kupitia Mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Kwaalinatu.

 ALIYEKUWA  mgombea Ubunge wa Chama Cha CUF mwaka 2015 Jimbo la Gando,Salim Mussa Omar na akajiunga na CCM miezi kadhaa iliyopita, akizungumza katika Mkutano huo wa kampeni na kumuombea kura Mgombea Uwakilishi wa Tiketi ya CCM kupitia Mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Kwaalinatu. 
MWAKILISHI wa Jimbo la Welezo Mhe. Hassan Khamis Hafidh  akizungumza katika Mkutano huo wa kampeni na kumuombea kura Mgombea Uwakilishi wa Tiketi ya CCM kupitia Mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Kwaalinatu.

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kusini Pemba Mhe. Faida Mohamed Bakari, akizungumza katika Mkutano huo wa kampeni na kumuombea kura Mgombea Uwakilishi wa Tiketi ya CCM kupitia Mkutano huo uliofanyika katika Uwanja wa Kwaalinatu.

 MGOMBE mteule Uwakilishi CCM Jimbo la Jang'ombe Ndugu Ramadhani Hamza Chande (kushoto) akisalimia na Mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete(kulia) katika kampeni za CCM.

 BAADHI ya  vijana wa CCM walioudhuria Mkutano huo wa kampeni wakisikiliza sera za Viongozi wa CCM.

 MSOMA Quraan akisoma maneno matukufu ya Mwenyezi Mungu kwa lengo la ufunguzi wa Mkutano huo.

 VIONGOZI mbali mbali wa CCM wakifuatilia matukio mbali mbali yanayofanyika katika Mkutano wa Hadhara wa kampeni za CCM katika Uwanja wa Kwaalinatu.

 WANA-CCM na wananchi kwa ujumla wakiimba wimbo wa mashujaa mara baada ya kuwasili mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi'.

  MGOMBE mteule Uwakilishi CCM Jimbo la Jang'ombe Ndugu Ramadhani Hamza Chande akimtuza msoma utenzi.


 KADA wa CCM ambaye pia ni Msaanii maarufu wa Bongo Movie  Issa Mussa 'Cloud' akimuombea kura mgombea wa CCM Jan'gombe.
  
MBUNGE wa Jimbo la Ubungo Mwita Waitara akizungumza na kumuombea kura Mgombea wa CCM Jan'ombe Ramadhan Hamza Chande.

 ALIYEKUWA  Kiongozo wa ngazi za juu  wa CUF, Julius Mtatiro na akajiunga na CCM, akimuombea kura mgombea wa CCM Ramadhan Hamza Chande.



 BAADHI ya viongozi na makada mbali mbali wa CCM wakiwa katika mkutano huo wa Kampeni.

 Mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akimuombea kura mgombea wa CCM Jimbo la Jang'ombe Ramadhan Hamza Chande kupitia mkutano wa kampeni za CCM.

 BAADHI ya viongozi wa CCM wakiwa katika mkutano huo.

 MGOMBEA Uwakilishi  tiketi ya CCM Jimbo la Jang'ombe akiwa katika picha ya Pamoja na Viongozi mbali mbali wa CCM, (PICHA NA IS-HAKA OMAR-AKZ). 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni