MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzaia Bara Ndugu Philip Mangulla akimkabidhi Bendera Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi katika Uchaguzi mdogo wa Jang'ombe Zanzibar. |
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi
wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa CCM Jimbo la Jang'ombe Zanzibar. |
MBUNGE wa tiketi ya CCM jimbo la Ukonga,Mwita Waitara akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni za CCM uchaguzi wa Jimbo la Jang’ombe Zanzibar. |
WANACHAMA wa CCM waliohudhuria
katika Mkutano huo wakishangilia mara baada ya kunadiwa kwa kuombewa kura Mgombea uwakilishi
wa CCM katika Jimbo hilo. |
MGOMBEA wa CCM nafasi ya
Uwakilishi Jimbo la Jang'ombe Ramadhan Hamaza Chande akizungumza na kuomba kura
kwa Wana-CCM na Wananchi mara baada ya kukabidhiwa miongozo na vitendea kazi vya CCM
ambavyo ni Ilani ya Uchaguzi, Katiba ya CCM na Bendera ya CCM mara baada ya
kunadiwa na kuombewa kura na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi. |
NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.
MAKAMU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Philips Mangulla amesema CCM imeendelea kuimarika kisiasa huku Vyama vya upinzani
vikiendelea kukosa mvuto na kudorora ambapo Wabunge na Madiwani wao wanajiunga na
CCM kwa nia ya kunufaika na Demokrasia iliyotuka inayopatikana ndani ya Chama
hicho.
Mwanasiasa huyo Mkongwe katika
Bara la Afrika na Tanzania kwa ujumla, alibainisha kuwa upinzani umekwisha poromoka
na kukosa ridhaa ya kuaminiwa mbele ya Wananchi, jambo linaloifa CCM iendelee
kutamba na kuonekana mahili na kinara wa Siasa za maendeleo.
Amesema katika kipindi cha Oktoba
mwaka huu Wabunge wa nne wamekwishavihama
vyama vyao hivyo vya upinzani na kujiunga na CCM.
Kauli hiyo ameitoa leo wakati akizindua rasmi kampeni za uchaguzi mdogo jimbo la Jangombe katika
uwanja wa Mwembe Matarumbeta mjini Unguja ambapo alisema wapo watu wanaosema
wabunge hao wananunuliwa lakini ukweli ni kuwa si hivyo.
Amesema aliyekuwa Mbunge wa jimbo
la Liwale ambaye alikuwa CUF, aliulizwa na uongozi wa CCM sababu ya kujiunga na
chama ambapo alidai kuwa alikuwa akipata tabu sana wakati wa utekelezaji wake
wa maendeleo ya jimboni kwake.
Katika maelezo yake alisema wananchi
wanakikubali chama cha CCM lakini jambo lilokuwa linampa tabu ni mipango ya
utekelezaji wa ahadi zake ambapo yote ambayo yanafanyika ni kutokana na ilani
ya CCM.
Mbali na hilo, amesema katika
uchaguzi huo wa jimbo la Jang’ombe wana-CCM wako 8000 huku wapinzani wakiwa
2500 hivyo ni dhahiriushindi ni wa CCM kinachotakiwa ni kuwa ni wanachama
kuwashawishi wapinzani kukiunga mkono katika uchaguzi wa Oktoba 27 mwaka huu.
Amesema kwa sasa Baraza la
Wawakilishi liko shwari na mambo yote yanakwenda ambapo watu wanajadili kwa
hoja maendeleo ya nchi na si kama awali ilivyokuwepo.
Amewasisitiza wanachama wa CCM na
Wananchi kwa ujumla kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua Mgombea wa CCM Ramadhan
Hamza Chande , ili aweze kuendeleza maendeleo na kutatua kero zitakazojitokeza
ndani ya Jimbo hilo.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Zanzibar
Dk.Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar ,Dk Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amesema uchaguzi huo mdogo wa jimbo wa Jangombe ni wa kujitathmni na kujipima kuelekea
2020.
Amesema ni wakati sasa wana-CCM kuungana kwa
pamoja na kujitokeza kwa wingi kwenda kuipigia kura CCM Oktoba 27 mwaka huu na
kwamba mgombea huyo ana sifa zote zinastahili kuwa mgombea.
"Ramadhani Hamza Chande ana
sifa na vigezo vyote vya kuiongoza Jang’mbe hadi kufikia mafanikio ya kuwa
Jimbo la mfano kwa maendeleo kwani bado ni kijana pia ana upeo na fikra za
mikakati ya maendeleo.
Kwa upande wake Mbunge wa tiketi
ya CCM jimbo la Ukonga,Mwita Waitara ameeleza kuwa kupitia uchaguzi huo mdogo lazima
CCM ioneshe kuwa upinzani umekufa kwa upande wa Zanzibar.
Ameongeza kuwa ni wakati sasa wanajangombe
kutoleta virusi katika Baraza la Wawakilishi ambapo ndio wenye kuleta vurugu
kwenye utendaji mzuri wa baraza hilo.
Katika maelezo yake Mbunge Waitara
amesema kuwa muungano wa vyama vya upinzani UKAWA ni wajanja na wezi kutokana
na kuwa wao wanapinga kila kitu hata
kama maendeleo yanafanyika.
Waitara amefafanua kuwa vyama vya upinzani
havitaki amani wala maendeleo na badala yake wanaleta vurugu hivyo uchaguzi huo
lazima CCM ioneshe kuwa upinzani wa CUF
umekufa.
Waitara amesema katika Chaguzi zote ndogo CCM
imeshinda kwa kishindo hivyo kwa upande
wa Zanzibar jimbo la Jangombe ushindi ni lazima kutokana na kuwa upinzani
umeshakufa.
Naye Mwenyenkiti wa CCM,mkoa wa
Mjini Talib Ali Talib, amesema uchaguzi huo
wa jimbo la Jangombe unatokana na uamuzi wa CCM
kufanya mabadiliko ya viongozi katika jimbo la Jangombe ambapo imemuondoa
kiongozi ambaye ni Mwakilishi wa jimbo hilo na kuamua kumweka kiongozi
mwingine.
Amesema CCM katika kampeni hiyo
itashinda na kwamba ni kawaida kwa chama kushinda uchaguzi wowote kutokana na utendaji
wake mpya wa chama chini ya viongozi wake makini.
Mwenyekiti huyo amesema Oktoba 27
mwaka huu wana-CCM wajitokeze wakampigie kura mgombea wa chama na kwamba
ushindi utakaopatikana utakuwa wa asilimia kubwa kutokana na wanajangombe kuwa
na uzoefu wa uchaguzi na haijawai kuchukuliwa na upinzani.
Naye Mgombea wa jimbo hilo la Jangombe
Hamza Ramadhani Chande ameahidi
wananchi wa jimbo hilo kutekeleza ilani ya
CCM kwa vitendo na kwamba bila ya kuwepo kwa ubaguzi.
Amesema atashirikiana na wananchi
wote kwa makundi ya vijana wanawake na wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kujadiliana
katika kutekeleza ilani hiyo kwa upande wa afya, elimu, miundombinu na vikundi
vya Ujasiriamali.
Pamoja na hayo aliongeza kuwa
atabuni mikakati mbadala katika ya kuhakikisha kila changamoto itakayojitokeza
inatafutiwa ufumbuzi wa kudumu kwa haraka kabla haijaleta madhara kwa jamii.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni