Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdulla Juma Saadalla akizungumza na vikundi sita vya
vijana wa CCM wa Vyuo vikuu na taasisi za
Elimu ya Juu Zanzibar, hapo
Afisi Kuu CCM Kisiwandui.
|
Baadhi ya vijana wa CCM wa Vyuo vikuu na
taasisi za Elimu ya Juu Zanzibar wakifuatilia kwa umakini nasaha
zinazotolewa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dkt. Abdulla Juma Saadalla.
|
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla “ Mabodi” amewataka wasomi na wataalamu wa CCM waliopo
katika taasisi za elimu ya juu kutumia taaluma zao kubuni mikakati endelevu
itakayosaidia kupunguza tatizo la ajira na kuimarisha uchumi wa nchi.
Rai hiyo ameitoa wakati akizungumza na vikundi sita vya
vijana na wasomi wa vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu wa Chama hicho nchini
huko Afisi kuu CCM Kisiwandui Zanzibar, Dkt. Mabodi amesema maendeleo ya taifa lolote
duniani yanatokana na fikra za
maendeleo zinazobuniwa na wasomi.
Amewambia wasomi hao wa kada mbali mbali za Vyuo Vikuu kuwa
ni lazima wakae pamoja na kupanga mikakati itakayoisaidia CCM na serikali zake
kupiga hatua za kimaendeleo katika nyanja mbali mbali za kiuchumi, kisiasa na
kijamii.
Ameeleza kuwa Chama Cha Mapinduzi kupitia sera zake
kinaendelea kutoa vipaumbele katika sekta za elimu hasa vyuo vikuu kuhakikisha
vinazalisha wasomi wenye uwezo wa kitaaluma utakaoisaidia
nchi kujitawala yenyewe kwa kila
sekta ili kuenzi kwa vitendo fikra za
waasisi wa Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964.
Aidha Dkt. Mabodi
amesema vijana hao ambao ni wataalamu
watumie nyenzo za kitaaluma zikiwemo fursa
ya ujasiriamali kwa kujiajiri wenyewe badala ya kusubiri ajira kutoka katika
katika chanzo kimoja cha nafasi za ajira kutoka serikalini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni