MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Samia Suluhu Hassan akipokea kadi ya kada ya CHADEMA katika hafla ya kupokea wanachama wapya 10 wa Chama hicho huko katika kijiji cha mtende mndo. |
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Samia Suluhu Hassan akijenga ofisi ya Tawi la Mtende Mndo, wakati akihitimisha ziara yake ya kichama Unguja. |
MAKAMU wa Rais, Samia Suluhu Hassani, ameivunja ngome ya mkoa wa kusini ya CHADEMA kwa kuwapokea Katibu wa Mkoa huo wa chama hicho ,Mjumbe wa Halmashauri kuu ya wilaya na wanachama 10 ambao wote wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Akiwapokea wanachama hao mara
baada ya kushiriki katika ujenzi wa ofisi ya Tawi la Mtende Mndo, Kusini Unguja katika ziara yake
alisema wanachama hao wameamua kufanya maamuzi hayo ya busara kutokana na kuona
CCM inavyotekelez ilani ya uchaguzi.
Makamu huyo wa Rais aliongeza
kuwa kurudi kwao CCM ni jambo la kuwapongeza hivyo kama walivyohaidi kutaka
kuwarejesha wenzao ndani ya chama wanapaswa kufanya hivyo.
"Mkataa kwao ni mtumwa hawa ni
wanachama ambao ukiwatizama hawana asili ya kuwa CHADEMA ingawa kuwa kwa mujibu
wa haki za binadamu wana haki za kuchagua chama
watakavyo,"alisema.
Alisema licha ya kuwa walikuwa kwenye
vikao vya chama hicho bado hawakuwa na tizamwa kwa jicho la ndani ama heshima.
Katika maelezo yake alisema
lazima wanachama hao wapya wapongezwe na kwamba lazima wapangiwe kazi na kufanya
kazi ya chama.
"Tumewapokea wanachama hawa
lakini tukumbuke kuwa chama sasa kinakusudia kufanya mabadiliko
makubwa ya kujitegemea na kwamba
huu ni mradi wa chama wa awamu ya tatu ambao tumeupitisha tangu mwaka 2010 hivyo
imenipa faraja ya kuona naweka jiwe ya msingi katika ofisi za
chama ambazo ujenzi wake umejitegemea,"alisema Makamu huyo wa Rais.
Aliongeza kuwa sasa muda umefika
wa kuzijenga ofisi nzuri za chama ambazo zina hadhi kuanzia kata hadi tawi na
kwamba zitatumika katika kujenga chama.
Makamu huyo wa Rais aliwataka wanachama
wa kusini kuwa na umoja ambao utasaidia kujenga chama na kwamba kuruhusu
mpasuko ni kuwapa mwanya wapinzani kupenya kirahisi.
Kwa upande wake aliyekuwa Katibu
wa CHADEMA wa mkoa wa Kusini, Unguja, Ally Othaman Shomari, alisema ameamua
kufanya uamuzi huo wa kujiunga na CCM kutokana na utekelezaji wake wa ilani.
Alisema awali CCM ilikuwa afanyi
vizuri kutokana na kuwa watu ambao mafisadi na kukipaka matope kwa wananchi.
"Lazima tuwe wa kweli kuwa
zamani CCM ilikuwa imeregarega lakini kwa sasa iko vizuri mimi niliondoka baada
ya wakati ule Dk.Wilbrod Slaa alivyokuwa akionesha udhaifu wa chama ulivyokuwa
hivyo baada ya chama kurudi kwenye mstari ndipo tumeamua kurudi,"alisema
Shomari.
Shomari aliongeza kuwa kwa upande wa Kusini
Unguja hakuna upinzani kwa sasa baada ya CCM kurudi kwa wananchi na kwamba
katika ofisi ya chama hicho hakuna aliyebaki wote wamerejea.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni