ENEO la shimo la choo cha Bi. Sania Zahor Omar mkaazi wa Magogoni kwa Mabata kilichoanguka kutokana na mvua zinazonyesha visiwani Zanzibar. |
VIONGOZI mbali mbali wa CCM wakikagua maeneo yaliyoathiriwa na maji ya mvua kutokana na baadhi ya wananchi kuziba mitaro ya kupitisha maji. |
VIONGOZI wa Chama cha Mapinduzi pamoja na Diwani wa wadi ya Pangawe ndugu Makame Pandu Mgana wakiangalia mitaro ya maji iliyozibwa na nyumba za makaazi ya wananchi katijka eneo hilo. |
BAADHI ya nyumba iliyoathiriwa na maji ya mvua zinazoendelea kunyesha uko Fuoni Chunga. |
MUONEKANO wa eneo lililojaa maji ya mvua katika mtaa wa Fuoni Chunga(Janga mizini) |
MUONEKANO wa eneo lililojaa maji ya mvua katika mtaa wa Fuoni Chunga(Janga mizini) |
NYUMBA zilizoathiriwa na maji Fuoni Chunga |
NYUMBA iliyoangukiwa na mti huko Dimani Tasaf ambayo mmiliki wake ni Ndugu Muhidin Khamis Muhidin. |
NYUMBA iliyoanguka ukuta kutokana na mvua zinazonyesha uko Mtoni kidatu juu ambayo mmiliki wake ni Makame Sheha Juma. |
KATIBU wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM Zanzibar Ndugu Bakari Hamad Khamis, akizungumza na Wana CCM na viongozi wa SMZ wa Mkoa Kusini Unguja katika ziara yake ya kukagua maeneo yaliyoathiriwa na mvua. |
MWENYEKITI wa CCM Mkoa wa kusini Unguja Ndugu Ramadhan Abdalla Ali akizungumza katika kikao cha dharura kabla ya kuanza ziara ndani ya Mkoa huo. |
MKUU wa Mkoa Kusini Ungua Hassan Hatib Hassan ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya siasa ya CCM Mkoa akitoa tathimini ya athari ya mvua ndani ya Mkoa huo. |
VIONGOZI mbali mbali wakiwemo WANEC na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa huo wakifuatilia kwa makini kikao hicho. |
MAAFISA kutoka Afisi Kuu ya CCM Zanzibar walioshirikim ziara hiyo wakifuatilia kwa makini masuala mbali mbali yanayofanyika katika kikao hicho. |
NYUMBA iliyoezuliwa na upepo inayomilikiwa na Seif Salum katika kijiji cha Paje Mkoa wa Kusini Unguja. |
MITI mbali mbali iliyong'olewa na upepo ulioambatana na mvua katika shehia ya Michamvi Mkoa wa Kusini Unguja. |
KITUO cha Afya cha Michamvi kilichoezuliwa na upepo. |
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) imeitaka serikali kuwachukulia hatua za
kisheria baadhi ya wananchi wanaojenga kwa makusudi katika mabonde na miundombinu
ya maji.
Pia imetaka baadhi ya viongozi wa wadi na
shehia ambao ni madiwani na masheha, wanaoshindwa kudhibiti ujenzi holela na
vitendo vya uharibifu wa mazingira katika maeneo yao, wawajibishwe kwa mujibu wa sheria.
Ushauri huo umetolewa na Katibu wa NEC, Idara ya Organazesheni CCM
Zanzibar Bakari Hamad Khamis, alipotembelea maeneo
yaliyoathiriwa na mvua za masika katika Mikoa ya Magharibi na Kusini Unguja.
Amesema wakati umefika wa Serikali kuondosha muhali na kuwachukulia
hatua kali za kisheria wananchi wanaoharibu miundombinu kwa makusudi na
kusababisha maji ya mvua kwenda sehemu zisizostahiki na hatimaye kusababisha
mafuriko.
Amebainisha kuwa maeneo mengi yaliyopata majanga hayo yameonekana kuathiriwa
na shughuli za kibinadamu zikiwemo uchimbaji wa mchanga, ujenzi holela na ukataji wa miti ovyo.
Amesema kila mwaka serikali imekuwa ikitoa tahadhari na kuwataka wananchi
waliojenga mabondeni wahamie maeneo salama lakini wamekuwa wakikaidi maelekezo
hayo.
Amezitaka manispaa hadi Serikali kuu kuratibu maeneo yote yenye historia
ya kupata mafuriko kila mwaka pamoja na kutafuta ufumbuzi wa kudumu juu ya
changamoto hiyo.
Kupitia ziara hiyo amesema CCM imetoa pole wananchi wote waliopata maafa
hayo na kuwataka kuwa wawe wavumilivu katika kipindi hiki kigumu na
kitaisimamia Serikali kupitia mfuko wa maafa itoe msaada wa haraka kwa wahanga
wa mafuriko hayo.
"CCM ipo bega kwa bega na wananchi wote waliopata maafa haya na
tutajitahidi kushirikiana na serikali kuhakikisha hatua za dharura hasa misaada
ya kibinadamu inawafikia walengwa.
Lakini pia wananchi nakuombeni sana tujenge utamaduni wa kujilinda na
kuchukua tahadhari juu ya matukio kama haya, kwani kuna baadhi ya sehemu
nimesikitika kuona nyinyi wenyewe ndio chanzo cha kusababisha mafuriko kutokana
na uharibifu wa mazingira na miundombinu mingine", amesema Bakari.
Ameuagiza uongozi wa CCM na UVCCM Mkoa Magharibi kwenda kumsaidia
shughuli za ujenzi wa nyumba Mwenyekiti wa CCM Tawi la Buyu Ndugu Matias
Theodori ambaye nyumba yake imeporomoka kutokana na mvua hizo.
Akitoa katika ziara hiyo Katibu wa CCM Mkoa wa Magharibi Aziza Mapuri,
amesema mvua zinazoendelea kunyesha katika Mkoa huo zinasababisha madhara
makubwa kwa wananchi na mali zao na Chama kipo karibu na wananchi wote
waliopata maafa hayo.
Naye Diwani wa wadi ya Pangawe Makame
Pandu Mgana ambaye wadi yake ni miongoni mwa sehemu zilizoathiriwa na mvua
hizo, amesema kwa kushirikiana na uongozi wa jimbo wanafanya juhudi za kuifanyia
matengezo mitaro iliyozibwa kwa shughuli za ujenzi na baadhi ya wananchi.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kusini Hassan Hatib Hassan, amesema jumla
ya nyumba 106 katika maeneo mbali mbali ya Mkoa huo zimeharibiwa na mvua
iliyonyesha April 16, mwaka 2018.
Amesema mbali na nyumba hizo kuna miti ya matunda na ya kawaida, migomba
pamoja na mazao ya kilimo yameharibiwa na mvua hizo zilizochanganyika na upepo.
Ameeleza kuwa katika juhudi za kuwafariji wananchi waliopata maafa hayo,
uongozi wa Mkoa unaendelea na juhudi ya kuratibu maeneo yote yaliyopata majanga
ili mamlaka inayohusika na masuala ya maafa iweze kuchukua hatua za haraka.
Akizungumza katika shehia ya Michamvi Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kusini
Unguja, Ramadhan Abdallah Ali amesema Chama Cha Mapinduzi katika Mkoa huo
kitaendelea kushirikiana na wananchi wote waliopata maafa hayo mpaka
watakaporudi katika hali za kawaida za kuendelea na harakati za kimaendeleo.
Maeneo yaliyotembelewa ni Magogoni kwa mabata, Pangawe, Fuoni jangamizi,
Fuoni chunga, Dimani Tasaf, Mtoni kidatu juu,Buyu pamoja na shehia ya michamvi
na Paje.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni