Jumamosi, 7 Aprili 2018

DK.SHEIN AONGOZA HITMA YA SIKU YA MASHUJAA, WANASIASA NA WANANCHI WAMSIFU MAREHEMU KARUME.


 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Abeid Karume katika hitma ya kuwaombea dua mashujaa wa Mapinduzi ya 1964 yaliyofanyika Kisiwandui Zanzibar.

MAKAMU wa Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Abeid Karume katika hitma ya kuwaombea dua mashujaa wa Mapinduzi ya 1964 yaliyofanyika Kisiwandui Zanzibar.
MWAKILISHI wa Jeshi la ulinzi Tanzania Meja Jenerali Sharif Sheikh Othman akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Abeid Karume katika hitma ya kuwaombea dua mashujaa wa Mapinduzi ya 1964 yaliyofanyika Kisiwandui Zanzibar.

 MWAKILISHI wa Mabalozi  ambaye ni balozi mdogo wa msumbiji Zanzibar  Jorges Agusto Menez akiweka  shada la maua katika  kaburi la marehemu Abeid Karume katika hitma ya kuwaombea dua mashujaa wa Mapinduzi ya 1964 yaliyofanyika Kisiwandui Zanzibar.
MWAKILISHI wa Baraza la Wazee wa CCM, Abdalla Rashid Abdalla  akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Abeid Karume katika hitma ya kuwaombea dua mashujaa wa Mapinduzi ya 1964 yaliyofanyika Kisiwandui Zanzibar.

 MWAKILISHI wa Familia ya marehemu Abeid Karume Balozi Ali Abeid akiweka shada la maua katika kaburi la marehemu Abeid Karume katika hitma ya kuwaombea dua mashujaa wa Mapinduzi ya 1964 yaliyofanyika Kisiwandui Zanzibar.

 VIONGOZI mbali mbali wa SMZ na SMT pamoja na familia ya marehemu Abeid  Aman Karume wakiomba dua mara baada ya kuhitimisha utaratibu wa kuweka maua katika kaburi la marehemu Abeid Aman Karume.

 WAZIRI  wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa na Afrika mashariki mhe. balozi Dkt. Agustino Maige(kushoto) akibadilishana mawazo na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi(kulia), katika hitma na dua ya mzee Abeid Karume na mashujaa wa Mapinduzi ya Zanzibar.
 MKE wa Rais wa kwanza wa Zanzibar Mama Fatma Karume akiwasili katika eneo la Kisiwandui kwa ajili ya hitma na dua katika siku ya mashujaa.



 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi(kushoto)  akisalimiana na Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar  Zubeir Ali Maulid(kulia) mara baada ya kuwasili kisiwandui kushiriki katika dua na hitma ya Siku ya mashujaa.

 MAKAMU wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd(kushoto) akisalimiana na WAZIRI  wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa na Afrika mashariki mhe. balozi Dkt. Agustino Maige(kulia), mara baada ya kuwasili kisiwandui kushiriki katika dua na hitma ya Siku ya mashujaa.
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi(kulia )akisalimiana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Idd(kushotomara baada ya kuwasili kisiwandui kushiriki katika dua na hitma ya Siku ya mashujaa.
 RAIS mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Ali Hassan Mwinyi(kushoto) akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi baada ya kuwasili katika hitma na dua ya kumbukumbu ya mashujaa.


  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi(kulia) akisalimiana na Rais mtaafu wa awamu ya sita Dkt. Aman Abeid Karume(kushoto), baada ya kuwasili katika hitma na dua ya siku ya mashujaa.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi(kulia) akisalimiana na  Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa (kushoto), baada ya kuwasili katika hitma na dua ya siku ya mashujaa.

 MAKAMU w Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwasili Kisiwandui kwa ajili ya hitma ya siku ya mashujaa.

 ENEO la Kaburi ya mzee Abeid Aman Karume lililopo Afisi Kuu ya CCM Zanzibar .

 VIONGOZI na wananchi mbali mbali wakiwa katika kisomo cha hitma ya siku ya mashujaa.
 RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk. Ali Mohamed Shein pamoja na viongozi wengine wa dini na serikali  wakiomba dua katika hitma ya siku ya mashujaa.



 WANANCHI mbali mbali walioudhuria katika kisomo cha hitma ya siku ya mashujaa





NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk.Ali Mohamed Shein ameongoza mamia ya wananchi wakiwemo viongozi mbalimbali katika kisomo cha hitma ya kumuombea kiongozi wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amani Karume na waasisi mbali mbali walioshiriki Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.

kisomo hicho kimefanyika Afisi Kuu ya CCM Zanzibar Kisiwandui na kuudhuriwa vingozi mbali mbali wa dini, serikali na wananchi kwa ujumla.

Akitoa mawaidha mara baada ya kumalizika kwa kisomo hicho, Ustadhi Khamis Gharib kutoka Ofisi ya Mufti mkuu wa Zanzibar alisema kuna mambo mazuri mengi ambayo kiongozi huyo ameyafanya.

"Tuna kila sababu ya kuwaombea viongozi awa sababu vitabu vya dini vinatueleza kuwa watu waliofanya mema muwalipe kwa wema kama hakuna jambo la kuwalipa basi tuwalipe kwa kuwaombea dua,"alisema 

Mara baada ya kisomo hicho na mawaidha hayo,viongozi mbalimbali waliweka mashada ya maua katika kaburi la kiongozi huyo ambapo walioongozwa na Rais,Dk.Shein.

Aidha,Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan aliweka shada la maua, ambapo familia ya marehemu iliwakilishwa na Balozi Ali Karume ambaye ni Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Mbali na hayo, Viongozi kutoka Serikali walihudhuria maadhimisho hayo akiwemo Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia Muungano na Mazingira, Januari Makamba.

Hitma hiyo pia ilihudhuriwa na baadhi ya viongozi akiwemo Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, Mke wa aliyekuwa Rais wa kwanza Zanzibar,Fatuma Karume.

Wengine waliohudhuria ni Rais mstaafu wa Zanzibar,Aman Abeid Karume,Rais Mstaafu wa awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi,Naibu Katibu Mkuu wa CCM ,Zanzibar, Dk.Abdulla Juma Sadala, Waziri wa Afya wa Zanzibar, Hamad Rashid.

Pia,viongozi wa dini walihudhuria ni Mufti wa Tanzania, Abubakar Zubeir Bin Ally na Sheikhe wa Mkoa wa Dar es Saalam, Alhad Mussa Salim.

Hayati Karume aliuwawa na wapinga mapinduzi Aprili 7, mwaka 1972 kwa kupigwa risasi katika jengo ilikuwa Makao Makuu ya Chama cha Afro-Shirazi (ASP), Kisiwandui,visiwani humu.

Mara baada ya hitma hiyo viongozi na wanachi walitoa maoni yao juu ya mambo mema yaliyoasisi wa marehemu mzee Abeid Karume.

Akizungumza Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Hamad Rashid Mohamed amesema Zanzibar inazidi kustawi kiuchumi kutokana na miongozi bora iliyoasisiwa na marehemu Karume.

Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Abdulla Juma Mabodi, ameeleza kuwa bila kujali tofauti za kisiasa wananchi wote wa Tanzania wa kila sababu ya kuenzi, kuthamini na kutathimi kwa kina mambo yote yaliyotekelezwa na mzee Karume na kasha kuyafanyia kazi kwa vitendo.

Naye Makamu Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Tabia Maulid Mwita akizungumza mara baada ya hitma hiyo amewasihi vijana kuiga uzalendo na uchapakazi wa marehemu mzee Abeid Karume kwani mema aliyoyafanya kwa visiwa vya Zanzibar , ni kielelezo tosha cha uzalendo wake.

Kwa upande wake mjane wa marehemu mzee karume, Mama Fatma Karume amesema kitendo cha serikali kuweka siku maalum ya kuwambea dua mashujaa wa Zanzibar walioshiriki Mapinduzi, ni utamaduni unaostahiki kuenziwa kwa maslahi ya vizazi vya sasa na vijavyo.

Naye Kassim Issa, mkaazi wa kijiji cha Makunduchi amesema mema yaliyofanywa na mzee karume enzi za uhai wake na kwa muda mfupi wa uongozi wake yatabaki kuwa ni alama na somo la kujitathimini kwa viongozi na wananchi kwa ujumla.









Hakuna maoni:

Chapisha Maoni