NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Mabodi akieleza mafanikio yaliyopatikaka kupitia utekelezaji wa Ilani ya CCM katika Sekta ya kilimo huko katika bonde la mpunga la Kizimbani. |
BAADHI ya wananchi na Wana CCM wakishiriki katika upandaji wa mpunga katika bonde la Kizimbani katika zira ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan. |
ENEO lililopandwa mpunga katika bongde la kizimbani katika ziara ya Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Hassan Suluhu iliyofanyika leo katika Mkoa wa Mjini. |
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan akielekea katika eneo la ufugaji wa kaa huko Fuoni Kibondeni. |
MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi Tawi la Fuoni kibondeni. |
MJUMBE wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM),
Samia Suluhu Hassan, ameridhishwa na kasi ya viongozi wa CCM ya kuresha
utamaduni wa kurudi kwa wananchi wa chini kusikiliza kero zao na kuzitafutia
ufumbuzi wa kudumu.
Amesema kwa kiasi kikubwa wananchi walikuwa
wamepoteza imani kwa CCM kutokana na kuwa viongozi wengi walikuwa wanatabia ya
kukaa ofisini n kutowafikia wananchi hao na kusikiliza changamoto zao
zinazowakabili.
Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na
wananchi wanaotumia bonde la mpunga la Kizimbani Unguja katika ziara yake ya
kutembelea miradi mbali mbali inayotekelezwa na
Wana CCM katika maeneo hayo ya kilimo cha mpunga.
Mhe.
Samia ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema kuwa ile dhana ya CCM mpya na Tanzania mpya imeanza kustawi
katika fikra za Wana CCM na kufanyiwa kazi kupitia utekelezaji wa ilani ya
uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2020/2015.
"CCM mpya imeanza kuonekana ikiwemo
kuwafuatilia wananchi wa chini zaidi kwa mfano katika mikakati ya kufuatilia
kaya maskini kwenye miradi ya TASAF viongozi wa chama wameanza kuonekana
kufuatilia utatuzi wa changamoto za kuondoa hali ya umaskini hivyo CCM iko
karibu na wananchi kwa sasa," amesema Makamu wa Rais.
Katika maelezo yake Makamu huyo wa Rais,
alisema ni ukweli kuwa chama cha siasa ni watu na kwamba chama hicho chochote
cha siasa kinapaswa kuwa karibu na wananchi kwani wao ndio walioiweka Serikali madarakani.
Amewataka viongozi na watendaji wa CCM
kukukumbushana kuwa pindi wanapopewa dhamana za uongozi hawatakiwi kukaa
maofisini bali wana majukumu ya msingi ya kuwaletea wananchi maendeleo.
Pia, aliwapongeza wanajumuiya wa wakulima wa
kilimo cha mpunga Kizimbani kwa juhudi zao za kuungana kwa jumuiya ambapo
itawasaidia kuweza kusaidiwa kwa urahisi kwa pamoja kwenye sekta ya kilimo
ikiwemo kupata mbolea kwa haraka.
Makamu wa Rais Samia ameahidi wanajumuiya
hiyo kuwasaidia kiasi cha fedha na kuwapatia trekta kupitia CCM ili kuisaidia
katika kilimo chao cha mpunga katika mabonde hayo mpunga ya Kizimbani na maeneo
mengine.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa CCM, Zanzibar,
Dk.Abdulla Juma Mabodi amesema Chama Cha Mapinduzi kinaendelea
kutatua kero za wananchi hatua kwa hatua
na kwa sasa kimesaidia kwa kiasi kikubwa wananchi wanaolima zao la mpunga
katika bonde la Kizimbani.
Dk. Mabodi ameeleza kuwa lengo la kuwasaidia
wakulima hao ni kukabiliana na changamoto za upungufu wa chakula hasa mchele
ambao wakulima wengi wamewekeza nguvu
zao katika kilimo cha mpunga.
Mapema Mbunge wa Jimbo la Bububu na anakaimu
Jimbo la Mtoni, Ndugu Mwatantakaje Haji Juma amesema kuwa bonde hilo lina
wakulima zaidi ya 700 kutoka jimbo hilo na maeneo ya jirani.
Ameeleza kuwa mradi wa kilimo kilimo cha
mpunga katika bonde hilo ni moja ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya
mwaka 2015/2020, ambayo viongozi mbali mbali wa jimbo wamekuwa wakitumia
rasilimali fedha kuunga juhudi za wananchi ambao ni wakulima wa zao la mpunga.
Kwa
upande wake Katibu wa Jumuiya ya Wakulima wa kilimo cha Mpunga Kizimbani,
Shafii Kibwana Said alimshukuru Makamu huyo wa Rais kwa hatua aliyoifanya
kuwafuata wakulima hao walioko chini kwa kuwasikiliza changamoto zao na
kuonesha nia ya kuzitatua.
Alisema matokeo ya faida walioanza kunufaika
nayo kupitia serikali ya CCM ni pamoja na kupata mbolea kwa gharama nafuu
ambapo wanajumuiya hiyo wanalipa asilimia 25 ya mbolea huku serikali ikiwalipia
asilimia 75.
Wakati huo huo ametembelea eneo la uhifadhi wa mazingira huko Fuoni Kibondeni na kushiriki
katika uvunaji wa kaa, ambapo awasifu juhudi za Jumuiya ya uhifadhi wa
mazingira kwa kupanda mikoko ambayo ni sehemu ya kulinda mazingira ya bahari.
Amesema kila mwananchi ana jukumu la kulinda
mazingira yasiharibiwe hivyo kitendo cha Wana CCM na wananchi kwa ujumla
kujitolea na kuhifadhi mazingira ni hatua muhimu inayotakiwa kuungwa mkono na
Chama pamoja na Serikali.
Akiendelea na ziara hiyo pia ameweka jiwe la msingi Tawi la Fuoni
Kibondeni , na kuwasisitiza wanachama wa Chama cha Mapinduzi kuendeleza
utamaduni wa kujitolea katika utekelezaji
miradi ya Chama.
Ameelezea kufurahishwa kwake na hatua
zilizofikiwa katika Tawi hilo ambalo chimbuko lake limetokana na Tawi la zamani
la ASP, lililozalisha wanachama wazalendo na wenye msimamo imara juu ya Chama
chao.
Mapema
Katibu wa CCM Mkoa wa Magharib Bi. Aziza Mapuri amemkabidhi taarifa ya
hali ya kisiasa ya Mkoa huo iliyoeleza mipango endelevu ya kuimarisha CCM
kisiasa, kiuchumi na kijamii itakayokiwezesha Chama hicho kushinda katika
uchaguzi Mkuu ujao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni