Ijumaa, 9 Machi 2018

KATIBU WA IDARA YA ORGANAIZESHENI ZANZIBAR ATEMBELEA JUMUIYA YA WAZAZI

Lengo la CCM ni kushinda Uchaguzi na sio vyengine. Kauli hiyo imesemwa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organaizesheni Zanzibar Nd. Bakari Hamad Khamis wakati alipofanya Ziara katika Afisi Kuu za Jumuiya ya Wazazi Zanzibar iliopo hapo Kikwajuni.
Amesema Chama kinapendelea kuwa na wanachama wengi ambao watapelekea kuzidi kuimarisha zaidi Hivyo ameshauri jumuiya kuwa makini pindi wanapoingiza wanachama kufanya hivyo kutapelekea mafanikio makubwa ndani ya chama pamoja na jumuiya zake.
Ameleza kuwa lengo la Ziara yake ni kujitambulisha kwao iliwaweze kutambuana na  kufanya kazi kwa pamoja na sio vyengine. Pia alisema kuwa lengo la Chama cha Mapinduzi ni kuhakikisha kuwa kinashinda katika kila Chaguzi. Kwani ndio madhumuni na Malengo ya Chama bila hivyo lengo la chama litakuwa halikutimia.  Hivyo sasa ni wakati muafaka wa kuanza kazi nasio kuzembea tu.
Nae Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa Nd. Najma Murtaza Giga amempongeza katibu kwa kuteuliwa kuongoza Idara hiyo ya Organaizesheni Zanzibar. Hivyo ameahidi kuwa watatoa ushirikiano katika kila jambo ambalo litakalo kuwa hitajika kusaidia na kumalizia kusema kwani lengo letu ni moja tu kuhakikisha chama kinaongoza Dola nasio vyenginevyo. 

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organaizesheni Zanzibar  Nd. Bakari Hamad Khamis akisaini kitabu cha Wageni mara tu baada ya kuwasli katika Afisi Kuu ya Jumuiya ya Wazazi Taifa iliopo  hapo Kikwajuni. (  Kulia ) Nd. Najma Murtaza Giga ambae ni Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa akimkaribisha katibu wa Idara ya Organaizesheni Zanzibar

Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wazazi Taifa akimkabidhi Katibu huyo taarifa ya utekelezaji wa jumuiya ya Wazazi

KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organaizesheni Zanzibar  Nd. Bakari Hamad Khamis akitoa nasaha zake kwa Watumishi wa Jumuiya ya Wazazi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni