Katibu wa Oganization CCM Zanzibar Nd. Bakari akizungumza na wanaCCM wa Tawi la Shaurimoyo ' B' |
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), Zanzibar, kimewataka viongozi wa wa chama visiwani humu kujipima katika utendaji wao wa kutoa huduma kwa wananchi.
Kauli hiyo ameitoa Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Organaizesheni,Zanzibar,Bakari Hamad Khamis wakati akizungumza
wanachama wa tawi la Shauri Moyo 'B', mjini Unguja alisema endapo inaridhisha iongezwe juhudi zaidi.
Alisema na kama viongozi hao utendaji wao haujiridhishi inapaswa kujiuliza sababu ambazo zinasababisha kutofanikiwa kufikia malengo
yaliowekwa.
"Lakini si viongozi pekee bali wanachama wote tunawajibika kufanya kazi hiyo kwa mantiki ya kuimarisha chama chetu pamoja na kuhudumisha
Zanzibar yetu,"alisema Katibu huyo
Katika maelezo yake Katibu Bakari alisema wanachama wanatakiwa kuwa wa moja ili kukijenga chama na kwamba endapo wakianza kuunga mkono hoja
za wapinzani hivyo kwa kufanya hivyo ni kutoisaidia Serikali ambayo inaongozwa na CCM.
"Sisi viongozi tunatakiwa tuelewe kuwa ni watu wa kwanza katika kukisimamia chama na kuisimamia Serikali kazi moja ya serikali ni
kutekeleza majukumu waliopewa na chama na ndio maana ikifika wakati wa uchaguzi tunaanda ilani,"alisema Katibu huyo
Aliongeza kuwa lazima wanachama wae na umoja ili kuhakikisha chama kinabaki kuendelea kushika dola na kuwatatulia matatizo wananchi na
kuwaletea maendeleo.
Katibu wa Oganization CCM Zanzibar Nd. Bakari akiwasili katika Tawi la Shaurimoyo ' B' kwa ajili ya kuzungumza na wanachama wa CCM Tawi hilo |
Katibu wa Oganization CCM Zanzibar Nd. Bakari akipokea risala kutoka kwa Nd. Arafa Juma Faki ambae ni Katibu wa CCM Tawi la Shaurimoyo ' B' |
Katibu wa Oganization CCM Zanzibar Nd. Bakari akizungumza na wanaCCM wa Tawi la Shaurimoyo ' B' |
Kaimu Katibu wa Wilaya ya Amani ambae pia ni Katibu wa Wazazi wilaya ya Amani Nd.Mwanaisha Ame Moh'd akitoa nasaha zake kwa Wanachama hao wa CCM wa Tawi la Shaurimoyo ' B' |
Add caption |
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni