Baraza la Wazee wa Chama Cha Mapinduzi Zanzibar kwa niaba ya wazee wote wa Chama hicho linampongeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk. Ali Mohammed Shein kwa kutimiza ahadi yake ya kuinua kiwango cha chini cha Mishahara 100% kwa watumishi wa Umma, hatua iliyoanzia mwezi wa April, 2017.
Pia wamemuomba Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi kuendelea kusimamia kwa umakini mambo yafuatayo:-
1.Kuwabana wasiolipakodi hasa baadhi ya wafanyabiashara wenye tabia za ukwepaji wa kodi hizo.
2. Kusimamia Bodi zinazoshughulikia masuala ya upandaji wa bei za bidhaa ili kuzuwia mfumko wa bei hizo zinazopanda bila ya kuzingatia kipato cha wananchi.
3. Pia, Afanye tathmini zitakazosaidia kusimamia rasli mali za Zanzibar ili zitumike kwa uangalifu zaidi kwa kuwanufaisha wananchi wote.
Aidha, tumefurahishwa na tukio la kupunguza kodi ya mapato kutoka kiwango cha asilimia 13% hadi asilimia 9% Lakini pia kusimamia na kuwajibisha watendaji wasio waaminifu kwa Serikali.
Pamoja na pongezi zetu wazee tunatoa nasaha kwa watumishi wa Umma kwa kuwaomba wafanye kazi kwa bidii na uadilifu. Mwisho sisi wazee tunawatakia mema wafanyakazi wa SMZ katika maisha yao na tunamuombea Mhe. Rais Dk. Ali Mohamed Shein na familia yake maisha mema, afya bora na mafanikio makubwa.
AHSANTENI SANA
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
MAPINDUZI DAIMA
CCM OYEE!
(KHADIJA JABIR)
MWENYEKITI WA BARAZA LA WAZEE WA CCM
ZANZIBAR
02/05/2017
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni