Jumatano, 31 Julai 2019

MHE.AMINA IDDI: AING'ARISHA UWT ZNZ KWA NYENZO ZA KISASA,ASEMA MASLAHI YA CCM YAWEKWE MBELE.

 MWAKILISHI wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi  Mhe.Amina Idd Mabrouk(wa pili kushoto) akikabidhi Komputa Moja kwa Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo(wa pili kulia) komputa hiyo kwa ajili ya Matumizi ya Ofisi ya Naibu Katibu Mkuu huyo.

 NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo(wa pili kulia) akimkabidhi Komputa Moja Katibu wa UWT Mkoa wa Magharibi Ndugu Zuwena Suleiman Mohamed (wa kwanza kushoto) kwa ajili ya Matumizi ya Ofisi ya Mkoa huo,iliyotolewa na  Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk(wa pili kushoto).

  NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo(wa pili kulia) akimkabidhi Komputa Moja Katibu wa UWT  Wilaya ya Mfenesini (wa kwanza kushoto Pili Issa Juma) kwa ajili ya Matumizi ya Ofisi ya Wilaya hiyo,iliyotolewa na  Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk (wa pili kushoto).

 NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo(kulia),akimkabidhi Komputa Moja Katibu wa UWT Wilaya ya Dimani Ndugu Sunna Said Mzee(wa kwanza kushoto),Komputa hiyo imetolewa na Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk(wa pili kushoto).

 MWAKILISHI wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk, akizungumza katika Hafla hiyo ya utoaji wa Komputa hizo, katika Hafla iliyofanyika Ofisi za CCM Kiembe Samaki Unguja.

 NAIBU Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo akizungumza katika Hafla ya utoaji wa komputa hiyo iliyofanyika katika Ofisi za CCM Kiembe Samaki Unguja.
 MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Magharibi Unguja akizungumza katika Hafla ya utoaji wa Komputa zilizotolewa na Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd iliyofanyika katika Ofisi za Chama Cha Mapinduzi Kiembe samaki Znz.

 VIONGOZI na Wanachama wa UWT wa Mkoa wa Magharibi wakiwa katika hafla ya kukabidhi komputa nne ya Mwakilishi wa Viti Maalum Mkoa wa Magharib ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk, iliyofanyika katika Ofisi za CCM Kiembe Samaki Unguja.


MWAKILISHI wa Viti Maalum Mkoa wa Magharibi ambaye pia ni Mbunge kupitia Baraza la Wawakilishi Mhe.Amina Idd Mabrouk,amewasihi Viongozi na Wanachama wa CCM kufanya Kazi za Chama Cha Mapinduzi kwa bidii ili kuandaa Mazingira rafiki ya Ushindi wa Mwaka 2020.  

Rai hiyo aliitoa wakati akikabidhi Komputa Nne zenye Thamani ya Shilingi Milioni Nane kwa Ofisi za UWT Zanzibar ambazo ni Afisi Kuu ya UWT Zanzibar, UWT Mkoa wa Magharib,UWT Wilaya ya Dimani na UWT Wilaya ya Mfenesini ambapo kila Ofisi imekabidhiwa komputa Moja,Hafla hiyo imefanyika katika Ofisi za CCM huko Kiembembe Samaki Unguja.

Mhe.Amina amesema ili Chama kishinde katika Uchaguzi Mkuu ujao kila mwanachama anatakiwa kuweka mbele maslahi ya CCM badala ya maslahi binafsi.

Katika maelezo yake Mhe.Amina, ameeleza kuwa Vifaa hivyo ni mwendelezo wa Utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020,ikiwa ni sehemu ya kutekeleza kwa vitendo ahadi alizozitoa kwa Wananchi.

Pamoja na hayo amewaahidi Akina Mama wa Mkoa wa Magharibi kuwa ataanzisha Vikundi vya Ujasiriamali ili kuwakwamua kiuchumi na waweze kujiajiri wenyewe na kuondokana katika wimbi la umaskini. 

Amewasihi  Viongozi na Wanachama wa UWT kuthamini juhudi za kimaendeleo zinazofanywa na Viongozi hao ili wazidi kupata nguvu na Uthubutu wa kutatua changamoto zinazowakabili Wananchi.

Akizungumza katika Hafla hiyo Mgeni rasmi Naibu Katibu Mkuu wa UWT Zanzibar Ndugu Tunu Juma Kondo,amempongeza  Mbunge huyo Mhe. Amina na Viongozi mbali mbali wa Mkoa huo ambao wamekuwa karibu na Wananchi kwa kutekeleza kwa Vitendo Ilani ya CCM.

 Ndugu Tunu, amewataka Viongozi na Watendaji waliokabidhiwa Komputa hizo kuzitunza vizuri ili zitumike kwa malengo yaliyokusudiwa katika kuhakikisha shughuli za kiutendaji za UWT zinatekelezwa kwa ufanisi zaidi.

Amesema Viongozi wa Chama na Serikali wanatakiwa kufuata nyayo za Viongozi Wakuu ambao ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli kwa katika kuwatumikia Wananchi kwa uadilifu.

Awali Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Magharibi Ndugu Zainab Ali Maulid,amesema Umoja na Mshikamano ndio siri ya mafanikio ya kuimarika kwa Umoja huo.
  


Jumapili, 14 Julai 2019

MHE.FAHARIA AKABIDHI VIFAA VYA TSH.MILIONI 15 KWA UWT MAJIMBO 9 YA MKOA WA MJINI.



MWENYEKITI wa UWT Mkoa wa Mjini Unguja Bi.Ghanima Sheha akifungua Kikao cha Baraza Kuu la Mkoa huo,huko katika Ukumbi wa Mkoa wa Mjini ulioopo Amani Unguja.

MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis  Shomari akizungumza na Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mjini kabla ya kukabidhi Vifaa.


BAADHI ya Wajumbe wa Baraza Kuu la UWT  Mkoa wa Mjini wakisikiliza nasaha za mgeni rasmi katika Ufunguzi wa Kikao cha Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mjini, kilichofanyika katika Ukumbi wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja.


MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis Shomari (kulia),akimkabidhi Viti 50 Katibu wa UWT Jimbo la Magomeni Ndugu Khadija Rajab Pazi (kushoto).

MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis  Shomari(kulia) akimkabidhi Viti 50 Katibu wa UWT Jimbo la Kikwajuni Ndugu Amina Hassan Suleiman.


MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis  Shomari(kulia) akimkabidhi Viti 50 Katibu wa UWT Jimbo la Malindi Ndugu Salma Said Muumin.

MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis  Shomari akimkabidhi Katibu wa UWT Wilaya ya Amani Ndugu Asha Mzee Kiti Kimoja na Meza Moja vya Ofisi.

 MWAKILISHI wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini ambaye pia ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakiklishi Zanzibar Mhe.Mgeni Hassan Juma,akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi Vifaa kwa Akina Mama wa UWT wa Majimbo 9 ya Mkoa wa Mjini.

 KATIBU wa UWT Mkoa wa Mjini Ndugu Stamili akitoa ufafanuzi wa masuala mbali mbali ya Kiutendaji katika Kikao cha Baraza Kuu la UWT  Mkoa huo kilichofanyika sambamba na kukabidhi Vifaa kwa Akina Mama.

 MWAKILISHI wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Mhe.Saada Ramadhan,akizungumza katika hafla hiyo.



MBUNGE wa Viti Maalum wa Mkoa wa Mjini Mhe.Faharia Khamis Shomari,amekabidhi Vifaa mbali mbali vyenye Thamani ya Shilingi Milioni 15 kwa Majimbo yote ya UWT ndani ya Mkoa huo.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Viti 451,Meza Moja ya Ofisi na  Mashine  Moja ya kutengenezea Chaki ikiwa ni sehemu ya kuunga Mkoa juhudi za Ujasiliamali za Akina Mama wa Mkoa huo.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi Vifaa hivyo Mbunge huyo Mhe.Faharia amesema lengo la kutoa Vifaa hivyo ni kutekeleza Ilani ya CCM ya Mwaka 2015/2020.

Mhe.Faharia ameeleza kuwa Akina Mama wa UWT ndani ya Mkoa huo pamoja na majukumu ya kisiasa waliyokuwa nayo bado wanatakiwa kujiajiri wenyewe kupitia ujasiriamali hivyo vifaa vilivyotolewa vitawasaidia katika harakati hizo za kujiajiri wenyewe.

Pamoja na hayo alitoa Wito kwa Wanawake wa rika mbali mbali ndani ya Mkoa wa Mjini kushiriki kaiunga Mkoa CCM ili ishinde katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mwaka 2020.

Katika hafla hiyo Wawakilishi wa Viti Maalum wa Mkoa huo ambao ni Mhe.Mgeni Hassan Juma ameahidi kutoa Mashine mbili za Photocopy kwa UWT Wilaya ya Amani na Mjini huku Mhe.Saada Ramadhan amekabidhi Mifuko Mitano ya Jipusamu kwa ajili ya kutengenezea chaki na kuahidi shilingi Milioni Moja kwa kila Wilaya zilizomo katika Mkoa huo.

Wakizungumza kwa wakati tofauti Makatibu wa UWT wa Majimbo yote yaliyomo katika Mkoa huo, wameahidi Vifaa hivyo kuvitunza na kuhakikisha wanavitumia katika matumizi yaliyokusudiwa.

Awali akifungua Kikao cha Baraza Kuu la UWT Mkoa wa Mjini Mwenyekiti wa Mkoa huo Ndugu Ghanima Sheha,amesema Kikao hicho kitajadili masuala mbali mbali ya kiutendaji na kutoa maelekezo ya kiutendaji juu ya ufanikishaji wa majukumu mbali mbali ya UWT na CCM kwa ujumla.