Ijumaa, 22 Februari 2019

WALIMU,WAZEE NA WALEZI WATAKIWA KUFUATILIA MIENENDO YA WANAFUNZI.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiweka Jiwe la Msingi na kufungua Shule ya Sekondari ya Michenzani iliyopo katika Jimbo la Mkoani Pemba katika ziara yake ya kuweka mawe ya msingi, kuzindua na kukagua miradi mbali mbali inayotekelezwa katika Wilaya ya Mkoani.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akikagua darasa lenye viti na meza za kisasa zilizonunuliwa nchini China na SMZ kwa lengo la kupunguza tatizo la upungufu wa madawati katika shule za msingi na Sekondari  nchini.

VITI na Meza za kisasa zitakazotumiwa na wanafunzi katika madarasa yaliyozinduliwa katika Shule ya Sekondari Michenzani Pemba.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi,wanafunzi na viongozi mbali mbali mara baada ya kuzindua madarasa ya kisasa kaika Skuli ya Sekondari Michenzani iliyopo Wilaya ya Mkoani Pemba.

NAIBU Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Mmanga Mgengo kitoa ufafanuzi wa mipango endelevu ya Serikali katika kuimarisha Sekta ya Elimu nchini huko katka hafla ya uzinduzi wa Skuli ya Ssekondari Michenzani.

MJUMBE wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu Lailah Burhan Ngozi pamoja na viongozi mbali mbali wa Chama na Serikali wakiwa Katika Hafla ya ufunguzi wa Shule ya Sekondari Michenzani Pemba iliyozinduliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein.

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Kusini Pemba Mhe.Faida Mohamed Bakari (aliyevaa nguo ya njano ya CCM akiwa na miwani) pamoja na viongozi mbali mbali katika hafla ya uzinduzi wa madarasa ya Sekondari Michenzani.

MJUMBE wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ndugu Mwanamkasi Rajab Aziz(aliyevaa mtandio mweusi) pamoja na wananchi mbali mbali wakiwa katika hafla ya uzinduzi wa madarasa ya shule ya Sekondari Michenzani Wilaya ya Mkoani Pemba.

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar ndugu Madina Mjaka akitoa maelezo ya kitaalamu juu ya ujenzi wa madarasa hayo katika shule ya Sekondari Michenzani.

MWALIMU Mkuu Masaidizi Shule ya Sekondari Michenzani Pemba Mwl.Wanu Is-haka Ngwali akizungumza katika Kipindi Maalum Cha 'KUTOKA KISIWANDUI' kinachofuatlia matukio mbali mbali katika ziara nzima ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Kisiwani Pemba.

BAADHI ya Wanafunzi wa Shule ya Sekondari na Msingi ya  Michenzani Pemba wakiwa katika hafla ya ufunguzi wa majengo mbali mbali katika shule hiyo,

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Mabodi akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi  Dk.Ali Mohamed Shein mara Baada ya Kuwasili katika uzinduzi wa majengo ya shule ya Sekondari Michenzani Pemba.
(PICHA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILINO AFISI KUU CCM ZANZIBAR)

NA IS-HAKA OMAR,PEMBA.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekitii wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amewakumbusha wazazi,walezi kushirikiana na walimu katika kufuatilia mienendo ya watoto wao pindi wanapokuwa shule na majumbani ili viwango vya ufaulu viongezeke zaidi. 

Dk.Shein amesema kwamba wanafunzi wanahitaji uangalizi wa hali ya juu kwa kila madau wa elimu ili kuhakikisha wanapata elimu bora na yenye kiwango kinachostahiki ili wafaulu vizuri katika mitihani yao ya shuleni na ya kitaifa kwa ujumla.

Rai hiyo ameitoa Dk.Shein katika  ufunguzi wa jengo la skuli ya sekondari Michenzani, Wilaya ya Mkoani Pemba, ikiwa ni ziara yake ya kwanza katika Wilaya za Pemba mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwa upande wa Unguja.

Dk.Shein ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, ameeleza kuwa elimu bora na viwango bora vya ufaulu wa wanafunzi wa ngazi mbali mbali za kielimu vitaongezeka endapo wananchi wataamua kushirikiana ipasavyo na Sekta ya elimu kwa kuwajengea watoto mazingira Rafiki ya kupenda kusoma kwa bidi.

Amesema walimu wana dhima kubwa katika kuwaendeleeza kielimu ya wanafunzi, hivyo akawataka kujikita katika kusomesha kwa kuzingatia maadili ya kazi zao.

Ameeleza kuwa  maendeleo ya nchi yoyote ile hutegemea upatikanaji wa elimu bora kwa wananchi wake, hivyo akasisitiza haja ya walimu kujikita katika ufundishaji na kuepuka kasoro zinarudisha nyuma kiwango cha elimu.

Amewasihi wanafunzi hao kusoma kwa bidi huku wakiepuka kufanya kazi au biashara hali ya kuwa wao bado ni wanafunzi. 

Amesema ni kazi ya Serikali kuwajengea mazingira bora wanafunzi kwa kuwapatia huduma zote muhimu, ikiwemo vifaa na madawati.

Ameeleza kuwa Serikali kununua madawati 44,000 kutoka nchini China, na kubainisha kuwa nusu ya samani hizo zimewasili na kugawiwa katika skuli mbali mbali Unguja na Pemba.

Naye Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mhe.Mmanga Mjengo Mjawili amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imeandaa mazingira bora ya kuwezesha wanafunzi kusoma kwa utulivu bila ya kuwepo na kikwazo chochote hatua inayotakiwa kupongezwa.

DK.SHEIN ASEMA UIMARISHAJI WA MITANDAO YA BARABARA UNATOKANA NA SERA ZA CCM.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiweka jiwe la Msingi katika ujenzi wa Barabara ya Mkanyageni-Kangani(KM5) ikiwa ni ziara yake Kisiwani Pemba katika Wilaya ya Mkoani.


BARABARA ya Mkanyageni-Kangani (KM5) iliyowekwa Jiwe la Msingi na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ziara yake Pemba ikiwa ni miongoni mwa kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Mkoani na majimbo jirani ya Wilaya ya Mkoani Pemba mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Barabara ya Mkanyageni-Kangani.

NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk.Abdulla Juma Saadalla Mabodi (kulia) pamoja na Waziri wa Nchi (OR) wa Zanzibar Mhe.Issa Ussi Gavu (kushoto)  na viongozi mbali mbali wakisikiliza na kufuatilia kwa makini nasaha za mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein  wakati akihutubia wananchi wa Wilaya ya Mkoani  Pemba.

WAZIRI wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar Dk. Sila Ubwa Mamboya akitoa ufafanuzi juu ya faida watakayoipata wananchi wa Wilaya ya Mkoani wanaotumia Barabara ya Mkanyageni-Kangani.

KATIBU Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Zanzibar  Mhe. Mustafa Aboud Jumbe akitoa maelezo ya kitaalamu juu ya ujenzi wa Barabara hiyo.

MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akiwa katika hafla hiyo ya uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa barabara Pemba.

MAELFU ya Wana CCM na Wananchi mbali mbali walioudhuria katika hafla ya uwekaji wa Jiwe la Msingi katika Barabara ya Mkanyageni-Kangani Pemba.
(PICHA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO AFISI KUU CCM ZANZIBAR.)



NA IS-HAKA OMAR,PEMBA.


MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein amesema Ilani ya CCM ya mwaka 2015/2020 imeeleza kwa ufasaha namna Serikali itakavyoimarisha miundombinu ya Barabara ili kuwarahisishia wananchi huduma za usafiri.

Amesema katika kutekeleza azma hiyo Serikali inaendelea kuimarisha mitandao ya barabara yenye viwango vya lami mijini na vijijini kwa lengo la kwenda sambamba na matakwa ya miongozo ya CCM kupitia Ilani ya uchaguzi ya Taasisi hiyo.

CRAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, amesema Serikali ina azma ya kujenga barabara mpya kutoka Chakechake hadi Mkoani, kutokana na umuhimu uliopo na kukidhi mahitaji ya wakati.

Ufafanuzi huo ameutoa mara baada ya kuweka Jiwe la Msingi katika Barabara ya Mkanyageni-Kangani(KM5) Wilaya ya Mkoani Pemba.


Dk. Shein ambaye pia ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi amesema amewataka wananchi wa maeneo mbali mbali katika wilaya hiyo kuitunza barabara hizo ili zidumu kwa muda mrefu.

Katika maelezo yake Dk. Shein ameeleza kuwaSerikali ina azma ya kujenga barabara mpya kutoka Chakechake hadi Mkoani, ili isaidie kurahisisha mitandao ya usafiri baina ya Wilaya hizo mbili ambazo ni kitovu cha biashara na shughuli za kijamii.


Amesema ujenzi wa barabara ya Mganyageni-Kangani uliainishwa katika Ilani ya mwanzo ya Uchaguzi wa mwaka 1965 ambapo Dk.Shein alikuwa ni mgombea uwakilishi kupitia jimbo hilo, na toka wakati huo serikali za awamu mbali mbali ziliandaa mazingira Rafiki ya kujenga barabara hizo kwa maslahi ya wananchi.

Aidha amesema Serikali ya SMZ kupitia CCM ilipoahidi kutenga barabara hizo wapo baadhi ya wananchi waliobeza ambao kwa sasa pia wananufaika na barabara hizo katika Maisha yao ya kila siku.

Dk.Shein amewasisitiza wananchi wa Wilaya hiyo kuacha kutumiwa na baadhi ya wanasiasa wanaopotosha kila jambo jema linalotekelezwa na Serikali.

Kupitia hotuba yake Dk.Shein amewasihi wananchi kuendeleza mshikamano na kuepuka migogoro isiyokuwa na manufaa kwa maendeleo ya wananchi wa Kisiwa cha Pemba.

Kupitia ziara ya Dk.Shein Kisiwani Pemba,  endelea kufuatilia Matangazo ya moja kwa moja mbashara(Live) kupitia Bahari FM Radio na Ukurasa wa Facebook wa Ikulu Zanzibar.