Jumamosi, 12 Septemba 2015

Dk. Shein akutana na wanafunzi wa shirikisho la Vyuo vya Elimu ya juu

Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein alikutana na wanafunzi wa vyuo vya Elimu ya juu. Hapo Afisi Kuu ya CCM Zanzibar. Leo mnamo 12/09/2015


Mhe. Dkt. Shein akionekana akisalimiana na Viongozi mbalimbali wa chama Kitaifa mara tu baada ya kuwasili hapo katika Afisi Kuu za Chama kwa ajili ya kuzungumza na wanafunzi wa Vyuo  vya Elimu ya Juu
Wanafunzi wa vyuo wakimpokea Mhe.Dkt. Ali Mohamed Shein. Wakionekana wakiimba na kucheka nyimbo za Chama 

Wanafuzi wakimpokea Dkt. Shein kwa shangwe na Vigelegele pindi tu alipowasili ndani ya ukumbi kwa ajili ya kupata nasaha zake


Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasili ndani ya Ukumbi wa CCM kwa ajili ya kuongea na wanafunzi wa shirikisho la vyuo 

Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein akiwasili ndani ya Ukumbi wa CCM kwa ajili ya kuongea na wanafunzi wa shirikisho la vyuo 

Mhe. Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanafunzi hao.


Jumatano, 2 Septemba 2015

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KIKAO CHA KAMATI MAALUM.

KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi imekutana leo, chini ya Mwenyekiti wake Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa Idara ya Organaizesheni, imesema kikao hicho cha kawaida kilifanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Mjini Zanzibar.

Taarifa imesema kikao pamoja na mambo mengine, kimewataka  Viongozi,  Watendaji na Wanachama wa CCM wa ngazi zote kufanya kazi kuhakikisha wagombea  wote  wa Chama hicho hasa wa Viti  vya Urais wa Zanzibar  Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli wanashinda kwa kishindo katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.

Kikao pia kimewataka Viongozi wa CCM wa ngazi zote  kuendeleza na kuimarisha mshikamano miongoni mwao hususan  wakati huu wa kuelekea kwenye kampeni na uchaguzi mkuu, ili ushindi uweze kupatikana.

Hadi sasa Chama Cha Mapinduzi kimesimamisha wagombea wake katika Majimbo yote 50 kwa nafasi ya Ubunge na 54 kwa nafasi ya Uwakilishi Visiwanni Zanzibar. Aidha, kimesimamisha  wagombea wake katika Wadi zote Unguja na Pemba.

Kikao pia kimeunda  Kamati  Kamati Ndogo ya Kampeni  yenye Wajumbe ishirini na moja (21) itakayoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif Ali Iddi na Katibu wake  ni  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai.

Wajumbe hao ni pamoja na :-


1.   Mhe. Balozi Seif Ali Iddi                   -           Mwenyekiti
2.   Mhe. Vuai Ali Vuai                           -           Katibu
3.   Mhe. Shamsi Vuai Nahodha                -           Mjumbe
4.   Mhe. Haji Mkema Haji                       -           Mjumbe
5.   Mhe. Hamad Yussuf Masauni             -           Mjumbe
6.   Mhe. Waride Bakari Jabu                   -           Mjumbe
7.   Mhe. Seif Shaaban Mohamed              -           Mjumbe
8.   Mhe. Najma Murtaza Giga                  -           Mjumbe
9.   Mhe. Dkt. Maua Abeid Daftari           -           Mjumbe
10.  Mhe. Prof. Makame M. Mbarawa      -           Mjumbe
11.  Mhe. Omar Yussuf Mzee                  -           Mjumbe
12.  Mhe. Ramadhan A. Shaaban              -           Mjumbe
13.  Mhe. Mohamed A. Mohamed            -           Mjumbe
14.  Mhe. Khadija Hassan Aboud              -           Mjumbe
15.  Mhe. Haroun Ali Suleiman                -           Mjumbe
16.  Mhe. Issa Haji Ussi Gavu                 -           Mjumbe
17.  Mhe. Mahmoud Thabit Kombo          -           Mjumbe
18.  Mhe. Shaka Hamdu Shaka                 -           Mjumbe
19.  Mhe. Balozi Ali Abeid Karume          -           Mjumbe
20.  Mhe. Moudline Castico                     -           Mjumbe
21.  Mwakilishi kutoka UWT                   -           Mjumbe