KAMATI Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi imekutana
leo, chini ya Mwenyekiti wake Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar wa
Idara ya Organaizesheni, imesema kikao hicho cha kawaida kilifanyika Afisi
Kuu ya CCM Kisiwandui, Mjini Zanzibar.
Taarifa imesema kikao pamoja na mambo mengine, kimewataka Viongozi,
Watendaji na Wanachama wa CCM wa ngazi zote kufanya kazi kuhakikisha
wagombea wote wa Chama hicho hasa wa Viti vya Urais wa Zanzibar Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein na Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Magufuli wanashinda kwa kishindo
katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25, mwaka huu.
Kikao pia kimewataka Viongozi wa CCM wa ngazi zote kuendeleza na kuimarisha mshikamano miongoni
mwao hususan wakati huu wa kuelekea
kwenye kampeni na uchaguzi mkuu, ili ushindi uweze kupatikana.
Hadi sasa Chama Cha Mapinduzi kimesimamisha wagombea wake katika
Majimbo yote 50 kwa nafasi ya Ubunge na 54 kwa nafasi ya Uwakilishi Visiwanni
Zanzibar. Aidha, kimesimamisha wagombea
wake katika Wadi zote Unguja na Pemba.
Kikao pia kimeunda Kamati
Kamati Ndogo ya Kampeni yenye
Wajumbe ishirini na moja (21) itakayoongozwa
na Mjumbe wa Kamati Kuu na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mhe. Balozi Seif
Ali Iddi na Katibu wake ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vuai
Ali Vuai.
Wajumbe hao ni pamoja na :-
1. Mhe. Balozi Seif Ali Iddi - Mwenyekiti
2. Mhe. Vuai Ali Vuai - Katibu
3. Mhe. Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
4. Mhe. Haji Mkema Haji - Mjumbe
5. Mhe. Hamad Yussuf Masauni - Mjumbe
6. Mhe. Waride Bakari Jabu - Mjumbe
7. Mhe. Seif Shaaban Mohamed - Mjumbe
8. Mhe. Najma Murtaza Giga - Mjumbe
9. Mhe. Dkt. Maua Abeid Daftari - Mjumbe
10. Mhe. Prof. Makame M. Mbarawa - Mjumbe
11. Mhe. Omar Yussuf Mzee - Mjumbe
12. Mhe. Ramadhan A. Shaaban - Mjumbe
13. Mhe. Mohamed A. Mohamed - Mjumbe
14. Mhe. Khadija Hassan Aboud - Mjumbe
15. Mhe. Haroun Ali Suleiman - Mjumbe
16. Mhe. Issa Haji Ussi Gavu - Mjumbe
17. Mhe. Mahmoud Thabit Kombo - Mjumbe
18. Mhe. Shaka Hamdu Shaka - Mjumbe
19. Mhe. Balozi Ali Abeid Karume - Mjumbe
20. Mhe. Moudline Castico - Mjumbe
21. Mwakilishi kutoka UWT - Mjumbe
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni