Ijumaa, 4 Oktoba 2019

WANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE CHUKWANI Z'BAR WAPEWA VYAKULA


 MWAKILISHI wa Viti Maalum Mhe.Amina Idd Mabrouk, akizungumza na Wanafunzi wa Kidato cha Nne wa Skuli ya Sekondari Chukwani waliopo katika kambi ya maandalizi ya kufanya Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne Mwaka huu.
WAKILISHI wa Viti Maalum Mhe.Amina Idd Mabrouk,(kushoto) akikabidhi Vyakula mbali mbali vikiwemo Mchele, Unga wa Ngano na Mafuta ya kula kwa Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari Chukwani Mohamed Abdallah Mohamed(kulia), kwa ajili ya Wanafunzi waliopo katika kambi ya maandalizi ya Mitihani ya Kidato cha Nne kwa Skuli hiyo.




WANAFUNZI wanaojiandaa kufanya Mitihani ya Taifa ya kidato cha Nne Mwaka huu, Visiwani Zanzibar wametakiwa kusoma kwa bidii  ili wafaulu  mitihani hiyo.

Wito huo umetolewa na Mwakilishi wa Viti Maalum Mhe.Amina Idd Mabrouk, katika mwendelezo wa ziara zake katika Mkoa wa Magharib,wakati akikabidhi Vyakula kwa Wanafunzi wa Kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari Chukwani kwa ajili ya kambi ya maandalizi ya mitihani  kwa mwaka huu.

Mwakilishi huyo amewasihi Wanafunzi hao kusoma kwa bidii ikiwa ni sehemu ya maandalizi rasmi ya kuwawezesha kufaulu.

Amesema wanafunzi hao wakifaulu vizuri watapata nafasi ya kuendelea na masomo ya ngazi za juu hadi kufikia Chuo Kikuu, hatua inayohitaji juhudi binafsi za kila mwanafunzi.

Pamoja na hayo amewasisitiza wanafunzi hao kuachana na vitendo visivyofaa hasa kushiriki katika masuala ya dawa za kulevya, mahusiano ya kimapenzi katika umri mdogo sambamba na matumizi mabaya ya simu.  

Akipokea Vyakula hivyo Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Sekondari Chukwani Mohamed Abdallah Mohamed, ameshukru kwa msaada huo na kueleza kuwa utawasaidia wanafunzi hao kupata Chakula kwa wakati na kupata muda wa kusoma vizuri katika kambi hiyo.

Mwl.Mohamed, amesema kuwa Uongozi wa Skuli hiyo umejipanga vizuri kwa kuwaanda vizuri wanafunzi hao 122 wanaotarajiwa kufanya Mtihani wa Kidato cha Nne kwa Mwaka huu.

Vyakula vilivyotolewa na Mwakilishi huyo ni pamoja na Mchele,Sukari, Unga wa Ngano pamoja na  Mafuta ya kula. 


Jumanne, 10 Septemba 2019

BI.CATHERINE-ASEMA SERA ZA CCM ZINAJALI HAKI ZA WATOTO.

VIONGOZI mbali mbali wakiwa katika ziara ya Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao(kulia),akimkabidhi zawadi Mdhamini wa Nyumba ya kulelea Watoto ya Mazizini Bi.Chumu Ali Abeid katika ziara hiyo ya Katibu Mwenezi.

 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao,akiwa amembeba Mtoto Hajra Abdillahi Abdalla aliyetupwa na Mama yake Kichakani baada ya kuzaliwa na akaokotwa na Mbwa hivi sasa analelewa na Serikali katika Nyumba ya kulelea Watoto Mazizini.

 KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao, akisalimiana na Watoto wanaolelewa katika Nyumba ya kulelea Watoto ya Mazizini.

 BAADHI ya Makatibu wa Siasa na Uenezi waliofuatana na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Catherine Peter Nao,katika ziara yake ya kutembelea Nyumba ya kulelea Watoto Mazizini Unguja. 


KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao(kulia),akimkabidhi zawadi Mdhamini wa Nyumba ya kulelea Watoto ya Mazizini Bi.Chumu Ali Abeid katika ziara hiyo ya Katibu Mwenezi.



KATIBU wa Kamati Maalum ya NEC,Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar Catherine Peter Nao, amesema CCM inasimamia vyema Ilani yake kwa kuhakikisha kundi la Watoto wanapata haki zao za msingi zikiwemo kupatiwa Malezi bora,Huduma bora za Afya,Elimu na kulindwa.

Kauli hiyo ameitoa katika ziara yake ya kumtembelea Mtoto Hajra Abdillahi Abdalla, aliyeokotwa na Mbwa baada ya Mama yake kumzaa na kumtupa kichakani huko Pemba miezi kadhaa iliyopita kwa sasa analelewa katika Kituo cha kulelea Watoto cha Mazizini Unguja.

Amesema CCM imeweka Sera bora na rafiki za kulinda maisha ya watoto ili wapate huduma muhimu zinazowawezesha Watoto kupata mazingira bora ya Kimalezi.

Akizungumzia Tukio la kutupwa kwa Mtoto Hajra, amesema vitendo vya aina hiyo vinatakiwa kupingwa vikali na jamii na yeyote atakayebainika achukuliwe hatua kali za kisheria kwani Mtoto anakuwa hana kosa lolote la kupelekea kutupwa.

Ameeleza kuwa Mtoto huyo aliyetupwa na Mama yake kichakani mara tu baada ya kuzaliwa kisha akaokotwa na Mbwa na kumpeleka sehemu salama za Watu ni kitendo cha kumshukru Mwenyezi Mungu.

Ameishukru Serikali kwa kuchukua hatua za haraka za kulinda Maisha ya Mtoto huyo sambamba na kumpatia huduma bora za kimalezi kama walivyo Watoto wengine katika Jamii.

Katibu huyo amewasihi Walezi wa Watoto hao katika Nyumba hiyo,kuhakikisha wanawalea katika Misingi bora ya Kimaisha hasa ya Kidini na kuwajengea mazingira ya kupenda kusoma ili watakapoanza kujitegemea wawe na uwezo wa kujimudu kimaisha.

Amewataka Watoto hao kujilinda dhidi ya Vitendo vya udhalilishwaji kwani kuna baadhi ya Watu wanatumia mbinu mbali mbali za kuwaadaa watoto kwa nia ya kuwadhalilisha.

Alitoa wito kwa Serikali kuendelea kuthibiti Vitendo vya Udhalilishaji kwani vinaharibu Maisha ya Watoto ambao ndio Viongozi na Wataalamu wa Taifa wa baadae.

Naye Mdhamini wa Nyumba ya kulelea Watoto Mazizini Bi.Chumu Ali Abeid, amewapongeza Viongozi hao kwa kutembelea Watoto wanaolelewa katika Nyumba hiyo.
Alisema kuwa hali ya Mtoto Hajra inaendelea Vizuri na kwa sasa anapewa huduma bora kwa uangalizi mkubwa hali inayochangia Afya yake kuimarika kila siku.

Katibu huyo alifuatana na Viongozi mbali mbali wakiwemo Wanawake wa UWT pamoja na Makatibu wa Siasa na Uenezi wa CCM Zanzibar, walitoa zawadi mbali mbali kwa Watoto wanaolelewa katika Nyumba hiyo.