BAADHI ya Wajumbe wa Baraza la UWT Wilaya ya Amani wakisikiliza nasaha za Mgeni rasmi, ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Mhe.Asha Abdalla Juma "Mshua' |
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa
wa Mjini Kichama Mhe.Asha Abdalla Juma ‘Mshua’,amewataka Wanawake katika Nchini
kuamini,kulinda na kuipigania CCM na kuhakikisha inashinda kwa kishindo mwaka
2020 kuliko Chaguzi zote zilizopita toka kuanzishwa Mfumo wa Vyama Vingi Mwaka
1992.
Amesema Serikali za Awamu
ya Saba ya Zanzibar pamoja na Serikali ya Awamu ya Tano ya Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania chini wa Marais wake ambao ni Dk.Ali Mohamed Shein na Dkt.John Pombe Magufuli Viongozi waliosimamia Vyema utekelezaji wa Ilani ya CCM.
Hayo ameyasema leo wakati akihutubia katika ufunguzi wa Baraza la UWT Wilaya ya Amani kilichofanyika katika Ofisi
za Wilaya hiyo Sebleni Amani Unguja.
Mhe.Asha amesema Serikali hizo zimeimarisha Huduma
za Afya,Miundombinu ya Barabara,Umeme,Elimu,Mikopo kwa Wanawake yenye masharti
nafuu pamoja na kutoa fursa za Uongozi
kwa Wanawake katika Chama na Serikali zote mbili.
Amesema Wanawake wanatakiwa
kuunganisha nguvu zao bila ya kujali bila ya kujali tofauti za Vyeo,rangi na
kabila wahakikishe CCM inashinda kwa ngazi zote katika Uchaguzi Mkuu ujao, hiyo
ndio itakuwa njia pekee ya kuthamini kwa vitendo juhudi zinazofanywa na Serikali.
Kupitia Mkutano huo
amewasihi Wajumbe hao kuendeleza Umoja na
Mshikamano katika kutekeleza majukumu yao ya kisiasa ndani na nje ya UWT, kwa
lengo la kuandaa mazingira rafiki ya kisiasa yatakayoimarisha CCM.
Amesema pamoja na majukumu waliyokuwa nayo Akina Mama hao pia wanatakiwa kuwalea Watoto katika
Maadili mema na kuhakikisha Wanakua Salama bila kufanyiwa Vitendo vya
Udhalilishwaji.
Akizungumzia suala
Uimarishaji wa Chama na Jumuiya hiyo, Mhe.Asha amesisitiza umuhimu wa kuongeza
Wanachama Wapya wenye Sifa kisheria za kuipigia kura CCM kwa kila Uchaguzi wa
Dola.
“Kila Mwanachama kwa nafasi
yake aanze kuwatafuta Wapiga kura Wapya wa makundi yote wenye Sifa za kupiga
kura, waelezeni mazuri mengi yanayopatikana ndani ya CCM japokuwa mengi
wanayaona na kuyatambua lakini bado tuna jukumu la kuwakaribisha kwa ukarimu
kwani CCM ni Chama cha Wote,,,Nyumbani kumenoga.”,amesema Mhe.Asha.
Kupitia Kikao hicho
Mhe.Asha,alikabidhi Komputa Moja na Printer Moja ya Kisasa ya rangi zenye Thamani ya Shilingi Milioni 1.5 kwa Uongozi
wa UWT Wilaya hiyo ili watekeleze kwa ufanisi shughuli mbali mbali za kiutendaji.
Naye Katibu wa UWT Wilaya
hiyo Ndugu Asha Mzee,akisoma taarifa ya Utendaji wa kazi za UWT, alisema
Viongozi,Watendaji na Wanachama wanashirikiana vizuri huku wakijipanga vizuri
kukabiliana na dalili zozote za upinzani ili CCM ishinde katika uchaguzi ujao.
Amesema katika mikakati ya
kuimarisha Jumuiya wamesimamia vizuri vikao vya ngazi za Matawi hadi Wilaya
kuhakikisha vinafanyika kwa mujibu wa Katiba sambamba na kufanya ziara,vikao na
mafunzo ya kuwajenge uwezo Akina Mama juu ya masuala mbali mbali ya kisiasa na
kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza Mjumbe wa
Mkutano huo ambaye pia ni Naibu Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar
Mhe.Mgeni Hassan Juma, aliupongeza Uongozi wa Wilaya hiyo kwa kutekeleza
masuala ya msingi ya kiutendaji yenye dhamira ya kuimasha UWT na Chama Cha
Mapinduzi kwa ujumla.
Kwa upande wake Mjembbe wa Mkutano huo ambaye pia ni Mwakilishi wa Viti Maalum kupitia Mkoa huo Mhe.Saada Ramadhan Mwendwa amesema Mkutano huo ulioambatana na Utoaji wa Mada mbali mbali za kuwajengea uwezo Viongozi wa Baraza hilo ili wakirudi katika maeneo yao watekeleze kwa ufanisi majukumu yao.
Kwa upande wake Mjembbe wa Mkutano huo ambaye pia ni Mwakilishi wa Viti Maalum kupitia Mkoa huo Mhe.Saada Ramadhan Mwendwa amesema Mkutano huo ulioambatana na Utoaji wa Mada mbali mbali za kuwajengea uwezo Viongozi wa Baraza hilo ili wakirudi katika maeneo yao watekeleze kwa ufanisi majukumu yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni