Mamia ya wananchi wa Zanzibar jana usiku walihudhuria katika Taarab Rasmi iliyoandaliwa na Chama Cha Mapinduzi kwa ajili ya kusherehekea mwaka mmoja tangu kuingia madarakani huko katika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi Kikwajuini Mjini Zanzibar.
Taarab hiyo iliyopigwa na Vikundi vya Culture, Big Star na Zanzibar One iliwafurahisha na wananchi wengi wakiwamo wanaCCM. Pamoja na Mgeni Rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambae pia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM - Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein
Mbali na Kiogozi huyo pia walikuwepo Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, wajumbe wa Halimashauri kuu CCM pamoja na Viongozi mbali vyama vya siasa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
Jumatatu, 27 Machi 2017
Ijumaa, 24 Machi 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, leo amekiongoza kikao cha Kamati Maalum
ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa..
Akizungumza
na vyombo vya habari Katibu wa Kamati
Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM wa Idara
ya Itikadi na Uenezi Mama Waride Bakari Jabu, amesema kikao hicho cha siku
moja kilifanyika Afisi Kuu ya CCM, Mjini Unguja.
Amesema
pamoja na mambo mengine, kikao kilipokea na kujadili majina ya wana CCM
waliojitokeza kuomba ridhaa ya Chama chao, ili waweze kuwania nafasi ya Ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki,
kwa kipindi cha mwaka 2017 - 2022.
Kikao
hicho kimefanyika kwa kuzingatia Ibara ya 114 (7) (b) ya Katiba ya CCM ya mwaka
1977, Toleo la 2012, ambayo inatoa
Mamlaka kwa Kamati Maalum ya H/Kuu yaTaifa ya CCM Zanzibar, kupokea na kujadili
na hatimaye kutoa mapendekezo yake kwa Kamati Kuu, kwa hatua zinazofuatia.
Amesema
jumla ya wana CCM 33, wakiwemo wanawake 7 na wanaume 26, kutoka Mikoa mbali mbali ya Unguja na Pemba, wamejitokeza kuomba waruhusiwe na CCM kugombea nafasi hizo.
Katibu
huyo wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya Itikadi na Uenezi amefafanua kuwa kwa
mujibu wa Katiba ya Jumuiya ya Afrika Mashariki,
Tanzania inapaswa kuwakilishwa na Wabunge tisa
(9).
Aidha
kikao hicho kilimtambulisha Ndugu. Abdullah Juma Saadalla (Mabodi) aliyepitishwa
na Mkutano Mkuu wa CCM hapo Machi 13, mwaka huu, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar. Aidha, kimeahidi kumpa kila aina ya mashirikiano ili aweze kutekeleza
majukumu yake aliyopewa na Chama
ipasavyo.
Kikao
pia kimewapongeza kwa dhati wana CCM hasa Vijana waliojitokeza kuomba kugombea nafasi hizo
muhimu za Uongozi katika Jumuiya ya
Afrika Mashariki hali inayoonyesha kuimarika kwa Demokrasia ndani ya Chama
hicho.
KIDUMU
CHAMA CHA MAPINDUZI.
Waride Bakari Jabu),
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,
Idara ya Itikadi na Uenezi - CCM,
ZANZIBAR.
24/03/2016.
Alhamisi, 23 Machi 2017
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kesho
(24/03/2017) anatarajia kukiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu
(NEC) ya Taifa ya CCM Zanzibar.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari
iliyotolewa na katibu wa Kamati Maalum ya NEC wa Idara ya Itikadi na Uenezi
Mhe. Waride Bakari Jabu, amesema kikao hicho maalum cha siku moja kitafanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui.
Amesema kwa kuwa kikao hicho ni maalum, kitakuwa na agenda
moja tu, ambayo ni kupokea na kujadili majina ya wana CCM waliojitokeza
kuchukua fomu za kugombea nafasi ya Ubunge
wa Bunge la Afrika Mashariki.
Kwa mnasaba huo, Katibu huyo wa Kamati Maalum ya NEC
Zanzibar amewataka Wajumbe wote wa kikao hicho kuwa wameshakaa kwenye viti vyao
ifikapo saa 3:30 barabara za asubuhi.
Kikao hicho kilitanguliwa na kikao cha Sekretarieti ya
Kamati Maalum ya NEC Zanzibar, iliyokutana leo
(23/03/2017) chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar
Mhe. Abdullah Juma Abdullah (Mabodi) kwa ajili ya kuandaa ajenda ya kikao
hicho.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
(Waride Bakari Jabu),
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC,
Idara ya Itikadi na Uenezi,
ZANZIBAR.
23/03/2017.
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)