Viongozi katika majimbo ya uchaguzi wametakiwa kujenga mshikamano na kuachana na makundi ambayo yamekuwa yakidhoofisha umoja wa wanachama katika utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi.
Hayo yalisemwa na katibu wa kamati maalumu ya halmashauri kuu ya CCM Zanzibar ya itikadi na uenezi Waride Bakari Jabu wakati alipozungumza na viongozi wa jimbo la Bububu mjini hapa.
Alisema mshikamano wa viongozi ikiwemo wawakilishi wabunge na madiwani unahitajika kwa kiwango kikubwa ili kufanikisha utekelezaji wa ilani ya CCM na kuondoa kero za wananchi katika majimbo.
'Chama cha mapinduzi kinakerwa na makundi ambayo yanadhoofisha maendeleo ya chama na kupiga hatua kubwa ya maendeleo'alisema.
Katika mkutano huo mwakilishi wa jimbo hilo Hussein Ibrahim Makungu maarufu Bhaa na mwakilishi wa mbnge wa jimbo hilo Sururu walitangaza rasmin kuzika tofauti zao na hitilafu zilizokuwepo awali huku wakielekeza nguvu kuhakikisha chama cha mapinduzi kinaendelea kushikilia jimbo hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni