CHAMA Cha Mapinduzi Zanzibar leo
kimemkabidhi Mwenyekiti wa Kamati ya Maafa Zanzibar Mhe. Mohamed Aboud Mohamed,
msaada wa bidhaa za vyakula vya aina mbali mbali vyenye thamani ya Tssh. milioni
ishirini na laki nne, kwa ajili ya wananchi walikumbwa na mafuriko katika
maeneo mbali mbali ya Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja.
Akikabidhi msaada huo, katika hafla
fupi iliyofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui, Naibu Katibu Mkuu wa CCM
Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai, alisema Chama hicho kimelazimika kuungana na
taasisi nyengine na watu binafsi walioguswa kutokana na janga hilo lililowapata
wananchi wa maeneo kadhaa ya Wilaya za Mjini na Magharibi ya Mkoa huo.
Msaada uliotolewa ni pamoja na mchele
polo (paketi) mia mbili (200), sukari, unga wa ngano, sabuni za kufulia (unga),
mafuta ya kupikia yaina ya korie, pamoja na fedha taslim shilingi milioni tano
(5,000,000/-).
Maeneo yaliyoathiriwa na mafuriko
hayo mkoani humo ni pamoja na Mpendae kwa Binti Amrani na Mpendae ya Migombani,
Mwanakwerekwe, Sebleni na Jang’ombe (Mjini), Kianga, Tomondo, Ziwamaboga na
Mtopepo (Magharibi) ambapo nyumba kadhaa zilibomoka kufuatia kujaa maji na
kuleta hasara kubwa.
“Chama Cha Mapinduzi ni chama
kinachowajali na kuwakumbatia wananchi, ndio maana tulilazimika kusitisha kikao
cha sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC Zanzibar,na kwenda kuwakagua na
kuwafariji wananchi wote siku iliyotokea mafuriko hayo”. Alisema Naibu Katibu
Mkuu huyo wa CCM Zanzibar na kuongeza kusema kuwa “CCM itafanya kila
linalowekana kuhakikisha wananchi wanapatiwa kila aina ya misaada, ili waishi
kama watu wengine”. Alidai Vuai.
Akitoa neon la shukrani, Mwenyekiti
wa Kamati ya Maafa ya Taifa (Zanzibar), ambaye pia ni Waziri Nchi (OMPR) Mhe.
Mohame Aboud Mohamed, ameelezea kufarajika kwake kutokana na msaada huo, ambapo
alisema umekuja katika wakati muafaka.
Amesema masaada huo kwa kiasi kikubwa
utatumika kama ulivyokusudiwa na kukidhi haja ya wananchi 102 waliopo katika kambini ya Mwanakwerekwe,
Wilaya ya Magharibi na kuongeza kusema kwamba idadi hiyo huenda ikaongezeka katika
siku zijazo.
Akizungumza na Watendaji wa Wizara ya
Majenzi pamoja na Manispaa, baada ya kutembelea maeneo yaliyokumbwa na mafuriko
hapo mei 5, mwaka huu, aliwataka kutekeleza
wajibu wao ikiwemo kusimamia na kuifanyia marekebisho mitaro ya maji
taka, ili iweze kupitisha maji kwa urahisi.
ufuatia hali hiyo, Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, amewaagiza Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni