Naibu Katibu
Mkuu wa CCM Zanzibar Ndugu Vuai ali Vuai amewataka viongozi na watendaji wa CCM
wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa Katiba inayopendekezwa inapigiwa kura ya
ndio na inapita hapo wakati wa kuuipigia kura ya maoni.
Naibu Katibu
Mkuu huyo aliyasema hayo leo huko Kendwa katika hoteli ya Palumbo wakati
alipokuwa anafungua mafunzo Elekezi kwa Watendaji na Viongozi wa Chama Cha
Mapinduzi wa Mikoa na Wilaya za Zanzibar.
Ndugu Vuai
aliwaeleza washiriki wa Mafunzo hayo Elekezi kuwa Chama chetu hivi sasa
kimekabiliwa na mambo makuu matatu likiwemo la kura ya maoni ya kupitisha
katiba inayopendekezwa na Uchaguzi Mkuu wa wa 2015 na tuhakikishe kuwa Chama cha
Mapinduzi kinashinda kwa kishindo ili kiendelee kuongoza Dola ya Tanzania.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni