Chama Cha Mapinduzi (CCM) ndio Chama pekee nchini chenye uwezo wa kudumisha amanina utulivu wa kitaifa, hivyo wananchi wana kila sababu ya kukichagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, ili kiendelee kuongoza dola.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa
CCM Zanzibar Ndugu Vuai Ali Vuai, alipokuwa akiwa hutubia wananchi wa Wilaya ya
Kusini Unguja kupitia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kiwanja cha mpira
cha Paje.
Amesema CCM ndio Chama pekee chenye sera,
dira na dhamira ya kweli ya kuwakomboa wanyonge wa taifa hili nakuwaletea maendeleo
endelevu ndani ya maeneo yao, hivyo wananchi wana kila sababu ya kukichagua na kukirejesha
tena madarakani katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Amesema kutokana na Utekelezaji kwa asilimia kubwa
wa Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 - 2015 sambamba na ahadi mbali mbali zilizowekwa
na Viongozi wa Chama hicho, wakati wa kampeni kuliko fanywa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, nidhahiri wananchi
watakiunga mkono CCM.
Akizungumzia kuhusu Katiba Pendekezwa, Naibu Katibu
Mkuu huyo wa CCM (Z) amewataka wana CCM kushikamana na kutumia muda ulisalia kabla
ya kura ya maoni, kutoa elimu kwa wananchi juu ya ubora wa Katiba hiyo, ili waweze
kuielewa na kuipigia kura wakati utakapowadia.
Amesema elimu hiyo itawasaidia kwa kiasi kikubwa
wananchi walio wengi kuwajengea uelewa mpana na hivyo kuipigia kura ya ndio Katiba
hiyo, hapo Aprili 30, mwaka huu.
Amesema Katiba hiyo imezingatia maslahi ya makundi
yote ya kijamii ya pande zote mbili za Muungano, kinyume na inavyopotoshwa na wanasiasa
wa vyama vya upinzani kwa kuweka mbele matakwa ya vyama vyao Zaidi kuliko wananchi.
Ametoa wito kwa Wana CCM hasa waliokuwa Wajumbe
wa Bunge la Katiba kutumia vikao vya Chama na mikutano ya hadhara kufafanua kwa
kina vipengele mbali mbali vya katiba hiyo, mbele ya Wana CCM na Wazanzibari wote
fursa zilizomo ndani ya katiba hiyo, kwani ndio mkombozi wao.
“Katiba hii Inayopendekezwa ndio mkombozi kwa
Watanzania hasa Wazanzibari kwa vile
inatoa fursa kubwa kwa uchumi na ustawi wa Zanzibar na wananchi wake,
hali inayopunguza kwa kiasi kikubwa yalemanung’uniko yaliyokuwepo ndani ya Katiba
ya mwaka 1977.
Amesema wapinzani wamekuwa mstari wa mbele kuibeza
Katiba hiyo, kutokana na ukweli kwamba walifahamu fika kuwa walikwisha shindwa hata
kabla ya kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba.
“Wanachokifanya viongozi wa ukawa ni kufitinisha wananchi watekeleze matakwa yao, ili waikatae, lakini CCM tunawaambia ya guju kamwe hawawezi kutimiza ndoto yao hiyo”.AlisisitizaVuai.
Alitumia nafasi hiyo kumpasha Mansour Yussuf Himid,
kutokana na madai yake ya kuwaonea uchugngu Wazanzibari, kwa kusema haina chembe
ya ukweli na iwapo angekuwa na uchungu wa kweli asingewanyang’anya wazalendo mapande
makubwa ya ardhi, majumba ya kuishi, mashamba, nk. Hivyo awarejeshee wenyewe.
Mapema,Naibu katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai,aliwakabidhi kadi za CCM jumla
ya wanachama wapya 113 waliojiunga na chama hicho, ikiwa ni juhudi ya viongozi
wa CCM wa wilaya hiyo ya awamu ya tatu ya mradi wa kuimarisha chama hicho.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni