CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema usimamizi mzuri wa kura za maoni ndani ya CCM ya kuwapata wagombea wa nafasi mbali mbali za uongozi katika vyombo vya dola ndio sila pekee itakayoleta ushindi wa Chama hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Kimesema iwapo Viongozi wa CCM watafanya uadilifu katika kutoa haki kwa wagombea wote waliojitokeza kuwania nafsi za uongozi ni wazi kabisa ushindi wa kishindo utapatika.
Hayo yamesemwa na Steven Kazidi Steven alipokuwa akiwailisha mada ya kanuni na sheria za uchaguzi mkuu katika vyombo vya dola ikiwa ni siku ya pili ya mafunzo elekezi ya viongozi wa CCM wa mikoa na wilaya za Zanzibar, huko Palumbo Hotel, Mkoa wa Kaskazini Unguja.
Amesema wakati umefika kwa Viongozi wa CCM hasa Watendaji hawana budi kuteua wagombea kwa misingi ya haki na uadilifu ili kukiletea CCM ushindi usioshaka katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu na hivyo kuendeleza wimbi la ushindi na kushika hatamu ya dola nchini.
Kidumu Chama Cha Mapinduzi
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni