Alhamisi, 8 Oktoba 2020
DK.MWINYI- ATAKA WAWEKEZAJI WACHANGIE MAENDELEO
DK.MWINYI-ASEMA ATATATUA CHANGAMOTO ZA WAWEKEZAJI
MGOMBEA urais wa Zanzibar kupitia
Chama cha Mapinduzi (CCM), Dk. Hussein Ali Mwinyi amesema akipata ridhaa ya
kuiongoza Zanzibar, ataweka misingi imara kwa wafanyabiashara ili wafanye
biashara zitakazoleta tija nchini.
Dk.
Mwinyi alisema hayo alipokuwa akizungumza na wafanyabiashara kusikiliza
changamoto zinazowakabili ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za mgombea huyo,
mkutano uliofanyika katika hoteli ya Golden Tulip, Malindi.
Alisema
sekta biashara ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi na kuongeza pato la taifa
hivyo atahakikisha anafungua milango ili wafanyabiashara waitumie kuimarisha
mifumo ya biashara.
Dk.
Mwinyi alisema ni vyema kwa wafanyabiashara wa ndani kuwa tayari kuitumia
milango hiyo kwa kufanya biashara kubwa ndani ya nchi na kutokaa pembeni kupoteza
fursa zitakazojitokeza.
“Ninagombea
nafasi hii, kwa lengo la kuwatumikia wananchi na wafanyabiashara ni sehemu
muhimu ya wananchi hivyo ninawaomba mjipanga vyema tukashirikiane na kwenda
sambamba na matakwa ya wanachi wetu,” alieleza Dk. Mwinyi.
Alisema
ili kufikia azma hiyo, serikali atakayoiongoza itashirikiana na jumuiya za
wafanyabiashara na kuangalia sheria, kanuni, masuala ya kodi na ukataji wa
leseni za biashara ili kuondoa vikwazo katika shughuli za biashara na viwanda
nchini.
Akizungumzia
sekta ya utalii, Dk. Mwinyi alisema ataiendeleza ili kuinua kiwango cha idadi
ya watalii wanaoingia nchini lakini pia kuongeza thamani na aina za utalii kama
njia moja wapo ya kuongeza mapato yanayotokana na sekta hiyo.
Alisema
pamoja na Zanzibar kuendelea kuwa sekta kiongozi katika kuchangia pato la
taifa, bado inapaswa kutangaza vivutio ilivyonavyo zikiwemo fukwe na kwa
kuwekewa mipango madhubuti itakayowavutia watalii kuongezeka.
Kwa
upande wa maendeleo ya viwanda, Dk. Mwinyi alisema sekta hiyo inahitaji mapinduzi
makubwa ili isaidia ustawi wa wananchi wote wakiwemo wawekezaji wazawa kuwekeza
kupitia sekta hiyo.
“Sekta
ya viwanda itakapoimarika, wakulima na wafanyabiashara wadogo wataweza kutumia
viwanda kwa kazi tofauti ili zilete tija kwao na taifa kwa ujumla,” aliemeza
Dk. Mwinyi.
Mapema
Akiwazungumza katika mkutano huyo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara
Zanzibar (ZNCC), Ally Amour, alisema serikali ya awamu ya saba imefanya mengi
kwa wafanyabiashara hali ambayo imepelekea kwa kiasi kikubwa kukua kwa uchumi
wa nchi.
Alisema
ni vyema anapoingia madarakani kiongozi huyo kusaidia kutayarisha mazingira
mazuri ya biashara ili nchi iweze kusonga mbele zaidi kimaendeleo.
Baadhi
ya washiriki wa mkutano huo, walimuomba kiongozi huyo kuzipa kipaumbele baadhi ya
changamoto zilizobakia hususani kupitia sekta ya kilimo kwa kukipa kipaumbele
kilimo cha umwagiliaji maji ili kuongeza uzalishaji utakaokidhi mahitaji ya
ndani chakula.
Mbali na hayo walimuomba akiingia
madarakani kulipatia ufumbuzi tatizo ufungaji wa maduka ya kubadilisha fedha za
kigeni ya watu binafsi kwani imechangia kuvuruga mfumo wa maisha na biashara za
baadhi nya wafanyabiashara wanaofanya shughuli hizo.