Jumatano, 14 Desemba 2016

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI.

MAKAMU Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi (BLM), Mhe. Dkt. Ali Mohamed Shein, kesho tarehe 15/12/2016 anatarajia kukiongoza Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa. 

Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo na Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Zanzibar - Idara ya Itikadi na Uenezi, Mhe. Waride Bakar Jabu, amesema kikao hicho cha kawaida cha siku moja kitafanyika Afisi Kuu ya CCM, Kisiwandui kuanzia saa 4:00 asubuhi. 

Amesema kikao pamoja na mambo mengine, kitapokea na kujadili Mapendekezo ya wanachama wa CCM wanaoomba kuteuliwa kugombea nafasi ya Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Dimani na kuongeza kuwa maandalizi yote yamekamilika.

Aidha, Katibu Waride amesema kikao hicho kilitanguliwa na Kikao cha Sekretarieti ya Kamati Maalum ya NEC, kilichokutana tarehe 14 Disemba, mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Mhe. Vuai Ali Vuai, kwa lengo la kuandaa Agenda za kikao hicho.

“KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI” 

Waride Bakar Jabu 
Katibu wa Kamati Maalum ya NEC 
Idara ya Itikadi na Uenezi - CCM 
ZANZIBAR
14/12/2016

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni