Jumanne, 28 Februari 2017
Jumanne, 14 Februari 2017
CCM yakabidhiwa Kombe la Ushindi
Na Mwandishi wetu,
ZIKIWA
zimetimia siku 10 tangu kuadhimishwa kilele cha kuzaliwa kwa Chama Cha
Mapinduzi(CCM), ambapo leo Timu ya Tawi la Chama hicho Kisiwandui imekabidhi rasmi Kombe
la ushindi kwa Katibu wa Kamati Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi
Zanzibar, Waride Bakar Jabu.
Hafla
hiyo imefanyika kufuatia ushindi wa Timu hiyo kwa njia ya penaliti 4-2 dhidi ya timu ya Wasanii wa muziki wa kizazi
kipya Zenj Fleva katika mechi ya shamrashara za kuadhimisha kuzaliwa kwa chama
hicho.
Akizungumza katika hafla hiyo Katibu wa Kamati
Maalum ya NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakar Jabu, amesema
licha ya CCM kufanya shughuli za Kisiasa bado inathamini mchango wa sekta ya michezo
katika kuharakisha maendeleo ya nchi.
Alisema
harakati za Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya mwaka 1964 zilifanywa na vijana
ambao wengi wao walikuwa ni wanamichezo mashuhuri katika vilabu vya timu za
hapa nchini.
Waride
alieleza kuwa ushindi waliotwaa timu ya Chama hicho ni miongoni mwa utekelezaji
wa matakwa ya Katiba ya CCM ibara ya 5 inayosisitiza ushindi kwa kila shughuli
inayofanywa chama hicho.
“Nakupongezeni
sana timu yetu kwa ushindi mliotwaa licha ya maandalizi ya mechi hiyo kuwa ya
muda mfupi, lakini kwa umoja na mshikamano wenu mmeweza kukijengea heshima
kubwa Chama katika sekta ya Michezo.
Nakuahidini
kuwa Chama chetu kitaendelea kuunga mkono juhudi zenu ili kuhakikisha taasisi yetu
inakuwa na timu ya mpira wa miguu yenye uwezo na nauomba uongozi wa timu
utafute mbinu ya kuanzisha timu za michezo mingine kwa lengo la kuweka uwiano
wa michezo kwa makundi yote”, .alieleza Waride.
Aidha
alisema kwa niaba ya Niaba ya Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai anatoa
wito kwa vijana kujiunga na michezo mbali mbali nchini kwa lengo la kuendeleza
heshima ya Zanzibar kimichezo.
Alisema
Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 inatambua umuhimu wa michezo katika
kukuza na kuinua uchumi na maendeleo ya nchi, hivyo ni miongoni mwa sekta
inayotakiwa kusimamiwa kikamilifu bila ya kuingiza mitizamo na itikadi za
kisiasa.
Amezitaka
taasisi zenye dhamana ya Michezo nchini kujitathimini na kufanya utafti
wa kuibua vikwazo vinavyopelekea kukwamisha juhudi za maendeleo ya
sekta hiyo na kutafuta ufumbuzi wa kudumu kwa maslahi ya wananchi wote.
Mapema
akisoma risala Afisa mwandamizi wa Masuala ya Michezo na Ufundi wa Timu hiyo,
Mzee Abdallah Khatib ameupongeza uongozi wa Afisi kuu wa kuwaunga mkono toka mwanzo
walipowasilisha wazo la kuundwa kwa timu itakayocheza mechi ya shamrashara ya
kuzaliwa kwa CCM.
Alieleza
kuwa pamoja na juhudi na umoja ulipo ndani ya timu hiyo bado wanakabiliwa na
changamoto ya ukosefu wa vifaa vya michezo zikiwemo mipira, jezi, koni, dawa za
matibabu (first Aids Kit) na usafiri wa kuwafikisha katika sehemu watakazokuwa
wanaenda kucheza mechi za kirafiki.
Naye
Meneja wa Timu hiyo Nadra Juma Mohamed alisema lengo la kuanzisha timu hiyo ni
kuendeleza umoja na ushirikiano baina ya ngazi mbali mbali za Chama na Jumuiya
ili kupata sehemu mbadala ya kubadilishana mawazo.
“
Tunaomba ushirikiano kutoka kwa viongozi wetu mbali mbali wakiwemo Wabunge,
Wawakilishi na Madiwani waje kutuunga mkono kwani jahazi tunalosafiria ni moja
katika kulinda maslahi ya chama chetu, huku tukiwa karibu na kundi la vijana
kimichezo.”, alisisitiza Meneja huyo.
Hata
hivyo, aliwashukru viongozi wa CCM na Taasisi mbali mbali zilizosaidia
kufanikisha mechi hiyo.
Mechi
hiyo iliyochezwa Februari 3 mwaka huu baina ya Timu ya Tawi la CCM Zanzibar
na Wasanii wa Zenj Fleva ambapo timu ya
Chama hicho ilitwaa Kombe, pea moja ya jezi na mpira mmoja wa miguu huku
wapinzani wao wakipata pea moja ya jezi.
Hafla
hiyo iliudhuriwa na Viongozi mbali mbali wa Chama na Jumuiya akiwemo
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Kichama Bora afya Silima Juma, Katibu wa
CCM Wilaya ya Mjini Fatma Juma Shomari, Katibu Msaidizi Jumuiya ya
Wazazi Zanzibar Mustafa Rashid Malwa, Kaimu Afisa Utawala Mkuu wa CCM
Zanzibar Mwenemzi Omar Said na Katibu wa Idara ya Organazesheni CCM
Zanzibar Haji Mkema Haji.
Ijumaa, 3 Februari 2017
CCM YAIBUKA KIDEDEA DHIDI YA WASANII
CCM yaibuka na Ushindi wa kishindo katika pambano lilichezwa leo hii katika Uwamja wa Amani.
Mpaka dakika 90 mpira ulikuwa Tawi la CCM Afisi Kuu 2-2 Wasani wa Kizazi kipya Zanzibar.
Baada ya hapo yapigwa matuta (penalti) na hatimae Tawi la CCM Afisi Kuu wakaipbuka kidedea kwa penalti 4-2 dhidi ya Wasani
Jisajili kwenye:
Machapisho (Atom)