Jumatatu, 11 Desemba 2017

VIONGOZI WA UMOJA WA VIJANA WA VYAMA VYA FRELIMO,ZANU PF, EFDD NA EFD WAVUTIWA NA SERA ZA CCM


NA IS-HAKA OMAR, DODOMA.

VYAMA rafiki wa Chama cha Mapinduzi, Rafiki wa Chama cha Mapinduzi vimeutaka Umoja wa Vijana Tanzania, kuutumia wakati huu wa awamu ya tano ya rais John Pombe Magufuli, kushirikiana na serikali yao ili kuwaletea watanzania maendeleo yao.

Wakitoa salamu zao viongozi wa Umoja wa Vijana kutoka chama cha Frelimo cha Msumbiji, Chama ha ZANU PF cha Zimbabwe, Chama cha EFDD cha Burundi na Shirika la Ujerumani EFD, walisema wanaipongeza serikali ya Tanzania kwa jitihada inazozichukua hivi sasa za kubadili maisha ya Watanzania.

Wamesema Tanzania hivi sasa imeonesha mfano mkubwa katika dunia katika kitekeleza vyema dhamira yake ya kuwapatia maisha bora watanzania na watakuwa tayari kuitangaza katika kiuwekezaji.

Mwakilishi kutoka Burundi, Inocent Havizirimbe, amesema  nchi yake iko tayari kushirikiana na Tanzania katika kuona wanaingia katika shughuli za uwekezaji, ambazo zitaweza kusaidia ajira kwa vijana.

Kutokana na hilo amewaomba vijana wa Tanzania kuisaidia nchi yao kuweza kufikia malengo yake ya mabadiliko na nchi yake itakuwa tayari kuungana nao.

Mwakilishi huyo, alisema tayari hivi sasa, imeshaingia mkataba na serikali ya Tanzania wa kampuni ya Jitegemee, ikiwa ni hatua itayoweza kufanyakazi pamoja na Watanzania.

Nae Mwakilishi kutoka nchini Zimbabwe, amesema  serikali ya nchi hiyo chini ya Rais mpya, iko pamoja na Chama tawala cha Tanzania katika kuhakikisha wanaendeleza umoja katika mataifa ya nchi za ukobozi.


Mwakilishi wa Chama cha Frelimo kutoka Msumbiji, ameeleza kuwa vijana wa Tanzania wanapaswa kuutumia vyema wakati huu kuona wanakisaidia Chama chao kwa kutambua wako katika mabadiliko ya vita dhidi ya rushwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni