Jumatatu, 31 Julai 2017

NITAENDELEA KUIMARISHA MIRADI MBALI MBALI



MBUNGE WA JIMBO LA KIWENGWA MHE. KHAMIS MTUMWA (UJISU) AMESWEMA ATAENDELEA KUIMARISHA MIRADI MBALI MBALI YA MAENDELEO KWA WANANCHI WA JIMBONI KWAKO MIRADI HIYO NI KATI YA MIKAKATI YA UTEKELEZAJI WA ILANI YA CHAMA CHA MAPINDUZI

Jumatatu, 17 Julai 2017

‘Mabodi’ ameshiriki katika mazishi ya watoto wanne waliofariki dunia jana baada ya kuingia kwenye gari iliyokuwa sehemu ya maegesho na likajifunga hali iliyopelekea watoto hao kukosa hewa na kufariki huko Kidongo Chekundu Unguja.

Na Is-haka Omar, Zanzibar. 

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ ameshiriki katika mazishi ya watoto wanne waliofariki dunia  jana  baada ya kuingia kwenye gari iliyokuwa sehemu ya maegesho na likajifunga hali iliyopelekea watoto hao kukosa hewa na kufariki huko Kidongo Chekundu Unguja.  

Marehemu hao waliotambuliwa kwa majina ya Mwatma Mohamed Malawi (2), Haisam Mustafa(2), Munawar Ahmed Khamis (3) na Muslim Hamza bakar (2) wote wamezikwa leo katika maeneo tofauti ya Makaburi ya Mwanakwere na Kiembe samaki Mbuyu Mnene Unguja. 

Akizungumza mara baada ya maziko hayo Naibu Katibu huyo huko katika makaburi ya Mwanakwerekwe, alisema CCM imepokea kwa masikitiko na mshituko mkubwa taarifa ya vifo vya watoto hao na inatoa mkono wa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa familia zilizopata msiba huo na kuwasihi waendelee kuwa wavumilivu kwa kipindi hiki cha msiba huo.

Alisema watoto hao walitarajiwa kuwa ni miongoni mwa viongozi na wataalamu wa fani mbali mbali wa baadae hivyo msiba huo umeacha pengo kubwa  kwa familia na taifa kwa ujumla.

Aidha Dkt. Mabodi aliwataka wazazi na walezi nchini kuwa karibu na watoto wao kwa kuhakikisha mazingira yanayotumiwa na watoto kucheza yanakuwa katika hali ya usalama ili kuepuka athari zinazoweza kusababisha majeraha ama vifo kwa watoto wao.

“ Kwa niaba ya CCM Zanzibar nawaomba wanafamilia wote wawe wavumilivu kwa kipindi hichi cha msiba huku vyombo vya ulinzi na usalama vikiendelea kufanya uchunguzi wa kina juu ya kubaini chanzo halisi cha vifo hivi na kutoa taarifa kwa umma.”, alisema Dkt. Mabodi.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya ndugu na wazazi wa marehemu hao walifafanua kuwa (jana) juzi majira saa 5:00 asubuhi watoto hao walikuwa wakicheza katika maeneo ya nyumbani kwao ghafla hawakuonekana mtaani hali iliyozusha hofu kwa familia za watoto wao na wakachukua juhudi za kuwatafuta katika maeneo mbali mbali hasa katika bandari na maeneo mengine kwa kuhofia kuwa wameibiwa na watu wasiojulikana.

Akieleza zaidi Bw. Ahmed Khamis ambaye ni baba mzazi wa mtoto aliyefariki  ambaye ni Munawar, alidai kuwa katika harakati za kuwatafuta watoto hao walifanikiwa kuwapata  majira ya saa 2:00 usiku wa july 16, Mwaka huu wakiwa ndani ya gari moja lililokuwa limeegeshwa katika maegesho ya gari za mtaani ambalo mmiliki wake aliliweka kwa muda mrefu na alikuwa amesafiri.

Bw. Ahmed alieleza kwamba baada ya hapo yeye kwa kushirikiana na majirani mbali mbali walishirikiana kuvunja milango ya gari hilo na kufanikiwa kuwatoa watoto hao wakiwa wamezimia na kupelekwa hospitali kuu yaMnazi Mmoja ambapo baada ya kufanyiwa vipimo na madaktari wakaambiwa kuwa tayari wamefariki dunia kutokana na kukosa hewa kwa muda mrefu.

Kwa mujibu wa maelezo ya shuhuda mmoja aliyehusika na harakati za kuwatoa watoto ndani ya gari walipokutwa wamefariki alisema mazingira yake yanaonyesha kuwa kabla ya watoto hao kufariki walikuwa wakichezea gari hilo na walipoingia ndani mlango ulijifunga na kushindwa kutoka nje hali iliyosababisha kukosa hewa na kufariki dunia.

Viongozi mbali mbali wa serikali na Chama Cha Mapinduzi waliudhuria katika mazishi hayo wakiwemo Katibu wa Kamati Maalum, Idara ya Itikadi na Uenezi CCM Zanzibar, Bi. Waride Bakari Jabu, Mbunge wa Jimbo la Jang’ombe  Ali Hassan Omar ‘King’ na  Waziri wa Kazi,uwezeshaji, wazee, vijana wanawake na watoto Maudline Castico.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt.Abdulla Juma Saadalla leo ameshiriki mazishi ya watoto nne waliofariki jana baada ya kuingia ktk gari iliyokuwa imeegeshwa mtaani kwao na ikajifunga hali iliyosababisha vifo vyao huko Kidongo chekundu Unguja.





Jumatatu, 10 Julai 2017

Hongereni sana wanaCCM na wale wote wapenda Amani

Mwenyekiti wa  Jumuiya ya wazazi Tanzania, Abdallah Bulembo amewataka wawakilishi, wabunge na madiwani wa majimbo ya Kusini Unguja  kuthamini kazi zinazotekelezwa na mabalozi wa nyumba kumi kwani wao ndio viongozi wanaolinda maslahi ya chama hicho kwa ngazi za chini.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza na viongozi na wanachama wa CCM wa Mkoa huo katika mwendelezo wa ziara  yake  ya kuimarisha uhai wa CCM Zanzibar, alisema  mabalozi wa nyumba kumi wanafanya kazi kubwa ya kutafuta wanachama hai  ambao ndio mtaji wa kisiasa wa kufanikisha ushindi wa chama hicho kwa kila uchaguzi.

Alieleza kuwa viongozi hao wa nyumba kumi ndio wanaowajua vizuri wanachama wenye uwezo na nia za kweli za kukisaidia chama hicho katika masuala mbali mbali za kisiasa hivyo wanatakiwa kuungwa mkono wakati wa utekelezaji wa majukumu yao.

Akizungumzia mabadiliko ya chama Bulembo alisema mabadiliko hayo  hayakufanyika  kwa kumkomoa  mtu bali yametokana na dhamira ya kukiimarisha chama kwa lengo la kuwapelekea wananchi wa mijini na vijijini maendeleo endelevu.

Alisema kutokana na mabadiliko yaliyofanywa ndani ya chama na kuweka utaratibu wa kugombea nafasi moja mtu mmoja ni moja ya mkakati wa kuhakikisha kila kiongozi anayepewa dhamana anatumikia nafasi yake kwa ufanisi .

“Wito wangu kwenu viongozi, watendaji na wanachama sote tushirikiane kufanya kazi za chama na jumuiya zetu kwa lengo la kutekeleza kwa vitendo dhana ya kuimarisha uchumi  ndani ya chama na kwa mwananchi mmoja mmojo”, alisema Bulembo.

 Aidha alifafanua kuwa malengo ya  CCM kupitia uchaguzi wa ndani ya chama unaoendelea hivi sasa ni kupata viongozi waadilifu watakaokuwa na uwezo wa kukemea vitendo vya rushwa na makundi yasiofaa ndani ya chama bila ya woga.

Bulembo ambaye ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, aliwasihi viongozi wa Chama hicho kutangaza mafaniko na fursa mbali mbali zilizofanywa na Chama Cha Mapinduzi kwa  kuimarisha  Sekta za elimu, afya na miundombinu ya usafiri wa anga, barabara na bandari za  kisasa..