Jumapili, 14 Oktoba 2018

MANGULA AFUNGUA RASMI KAMPENI ZA CCM UCHAGUZI JANG'OMBE , WAITARA ATAJA SABABU ZA KUONDOKA UPINZANI.


 MBUNGE wa Jimbo la Jang'ombe Ndugu Ali Hassan King(kulia) akimkabidhi Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020 kwa niaba ya CCM Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi katika Jimbo hilo Ndugu Ramadhan Hamza Chande(kushoto), makabidiano hayo yamefanyika mbele ya Makamu Mwenyekiti wa CCM Ndugu Philip Mangulla.

 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzaia Bara Ndugu Philip Mangulla(katikakati) akimkabidhi Katiba ya CCM ya mwaka 1977 toleo la 2017, Mgombea Uwakilishi wa CCM ndugu Ramadhan Hamza Chande katika Mkutano wa Hadhara wa uzinduzi wa Kampeni za CCM uliofanyika katika uwanja wa Mwembe Matarumbeta uliopo katika Ofisi za CCM jimbo la Jang'ombe.

 MAKAMU Mwenyekiti wa CCM Tanzaia Bara Ndugu Philip Mangulla akimkabidhi Bendera Mgombea wa nafasi ya Uwakilishi katika Uchaguzi mdogo wa Jang'ombe Zanzibar.

 NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla 'Mabodi' akizungumza katika mkutano huo wa uzinduzi wa kampeni za Uchaguzi Mdogo wa CCM Jimbo la Jang'ombe Zanzibar.

 MBUNGE wa tiketi ya CCM jimbo la Ukonga,Mwita Waitara akizungumza katika uzinduzi wa Kampeni za CCM uchaguzi wa Jimbo la Jang’ombe Zanzibar.                                          

 WANACHAMA wa CCM waliohudhuria katika Mkutano huo wakishangilia mara baada ya kunadiwa kwa kuombewa kura  Mgombea uwakilishi wa CCM katika Jimbo hilo.
 MGOMBEA wa CCM nafasi ya Uwakilishi Jimbo la Jang'ombe Ramadhan Hamaza Chande akizungumza na kuomba kura kwa Wana-CCM na Wananchi mara baada ya kukabidhiwa miongozo na vitendea kazi vya CCM ambavyo ni Ilani ya Uchaguzi, Katiba ya CCM na Bendera ya CCM mara baada ya kunadiwa na kuombewa kura na viongozi mbali mbali wa Chama Cha Mapinduzi.


NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

MAKAMU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philips Mangulla amesema CCM imeendelea kuimarika kisiasa huku Vyama vya upinzani vikiendelea kukosa mvuto na kudorora  ambapo Wabunge na Madiwani wao wanajiunga na CCM kwa nia ya kunufaika na Demokrasia iliyotuka inayopatikana ndani ya Chama hicho.

Mwanasiasa huyo Mkongwe katika Bara la Afrika na Tanzania kwa ujumla, alibainisha kuwa upinzani umekwisha poromoka na kukosa ridhaa ya kuaminiwa mbele ya Wananchi, jambo linaloifa CCM iendelee kutamba na kuonekana mahili na kinara wa Siasa za maendeleo.

Amesema katika kipindi cha Oktoba mwaka huu Wabunge wa nne  wamekwishavihama vyama vyao hivyo vya upinzani na kujiunga na CCM.
Kauli hiyo ameitoa leo  wakati akizindua rasmi kampeni  za uchaguzi mdogo jimbo la Jangombe katika uwanja wa Mwembe Matarumbeta mjini Unguja ambapo alisema wapo watu wanaosema wabunge hao wananunuliwa lakini ukweli ni kuwa si hivyo.

Amesema  aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Liwale ambaye alikuwa CUF, aliulizwa na uongozi wa CCM sababu ya kujiunga na chama ambapo alidai kuwa alikuwa akipata tabu sana wakati wa utekelezaji wake wa maendeleo ya jimboni kwake.

Katika maelezo yake alisema wananchi wanakikubali chama cha CCM lakini jambo lilokuwa linampa tabu ni mipango ya utekelezaji wa ahadi zake ambapo yote ambayo yanafanyika ni kutokana na ilani ya CCM.

Mbali na hilo, amesema katika uchaguzi huo wa jimbo la Jang’ombe wana-CCM wako 8000 huku wapinzani wakiwa 2500 hivyo ni dhahiriushindi ni wa CCM kinachotakiwa ni kuwa ni wanachama kuwashawishi wapinzani kukiunga mkono katika uchaguzi wa Oktoba 27 mwaka huu.
  
Amesema kwa sasa Baraza la Wawakilishi liko shwari na mambo yote yanakwenda ambapo watu wanajadili kwa hoja maendeleo ya nchi na si kama awali ilivyokuwepo.

Amewasisitiza wanachama wa CCM na Wananchi kwa ujumla kufanya maamuzi sahihi ya kumchagua Mgombea wa CCM Ramadhan Hamza Chande , ili aweze kuendeleza maendeleo na kutatua kero zitakazojitokeza ndani ya Jimbo hilo.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM,Zanzibar Dk.Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar ,Dk Abdulla Juma Saadalla ‘Mabodi’ amesema uchaguzi huo mdogo wa jimbo wa Jangombe ni wa kujitathmni na kujipima kuelekea 2020.

Amesema ni wakati sasa wana-CCM kuungana kwa pamoja na kujitokeza kwa wingi kwenda kuipigia kura CCM Oktoba 27 mwaka huu na kwamba mgombea huyo ana sifa zote zinastahili kuwa mgombea.

"Ramadhani Hamza Chande ana sifa na vigezo vyote vya kuiongoza Jang’mbe hadi kufikia mafanikio ya kuwa Jimbo la mfano kwa maendeleo kwani bado ni kijana pia ana upeo na fikra za mikakati ya maendeleo.

Kwa upande wake Mbunge wa tiketi ya CCM jimbo la Ukonga,Mwita Waitara ameeleza kuwa  kupitia uchaguzi huo mdogo lazima CCM ioneshe kuwa upinzani umekufa kwa upande wa Zanzibar.

Ameongeza kuwa ni wakati sasa wanajangombe kutoleta virusi katika Baraza la Wawakilishi ambapo ndio wenye kuleta vurugu kwenye utendaji mzuri wa baraza hilo.

Katika maelezo yake Mbunge Waitara amesema kuwa muungano wa vyama vya upinzani UKAWA ni wajanja na wezi kutokana na kuwa  wao wanapinga kila kitu hata kama maendeleo yanafanyika.

Waitara amefafanua kuwa  vyama vya upinzani havitaki amani wala maendeleo na badala yake wanaleta vurugu hivyo uchaguzi huo lazima  CCM ioneshe kuwa upinzani wa CUF umekufa.

 Waitara amesema katika Chaguzi zote ndogo CCM imeshinda kwa  kishindo hivyo kwa upande wa Zanzibar jimbo la Jangombe ushindi ni lazima kutokana na kuwa upinzani umeshakufa.

Naye Mwenyenkiti wa CCM,mkoa wa Mjini Talib Ali Talib, amesema uchaguzi  huo wa jimbo la Jangombe unatokana na uamuzi wa CCM  kufanya mabadiliko ya viongozi katika jimbo la Jangombe ambapo imemuondoa kiongozi ambaye ni Mwakilishi wa jimbo hilo na kuamua kumweka kiongozi mwingine.

Amesema CCM katika kampeni hiyo itashinda na kwamba ni kawaida kwa chama kushinda uchaguzi wowote kutokana na utendaji wake mpya wa chama chini ya viongozi wake makini.

Mwenyekiti huyo amesema  Oktoba 27 mwaka huu wana-CCM wajitokeze wakampigie kura mgombea wa chama na kwamba ushindi utakaopatikana utakuwa wa asilimia kubwa kutokana na wanajangombe kuwa na uzoefu wa uchaguzi na haijawai kuchukuliwa na upinzani.

Naye Mgombea wa jimbo hilo la Jangombe Hamza Ramadhani Chande  ameahidi wananchi wa jimbo hilo kutekeleza ilani ya  CCM kwa vitendo na kwamba bila ya kuwepo kwa ubaguzi.

Amesema atashirikiana na wananchi wote kwa makundi ya vijana wanawake na wanafunzi wa vyuo vikuu kwa kujadiliana katika kutekeleza ilani hiyo kwa upande wa afya, elimu, miundombinu na vikundi vya Ujasiriamali.

Pamoja na hayo aliongeza kuwa atabuni mikakati mbadala katika ya kuhakikisha kila changamoto itakayojitokeza inatafutiwa ufumbuzi wa kudumu kwa haraka kabla haijaleta madhara kwa jamii.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni